IQNA

Israel kubomoa msikiti Quds Mashariki

18:44 - August 24, 2015
Habari ID: 3351059
Utawala haramu wa Israel umeamuru kubomolewa milki tatu zaidi za Wapalestina, ukiwemo msikiti mmoja ulioko Quds Mashariki.

Majdi al Abbas Afisa wa Kipalestina wa Kitengo cha habari cha Wadi Hilweh huko Silwan amesema kuwa maafisa wa manispaa wa Israel wameamuru kubomolewa jengo moja na nyumba iliyoko katika eneo hilo.
Msikiti wa al Qaaqaa ambao Israil imeagiza ubomolewe ulijengwa miaka mitatu iliyopita. (Msikiti huo una ukubwa wa mita mraba 110 na ukiwa na uwezo wa kuchukua waumini 5000.) Mapema wiki hii mahakama moja ya utawala wa Kizayuni wa Israel ilitoa amri ya kubomolewa uwanja wa mpira na bohari moja huko katika eneo la Silwan. Silwan ni moja ya maeneo ambako raia wa Palestina wamekuwa wakifukuzwa kwa nguvu majumbani mwao na Israel ili kutoa mwanya kwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni...mh

3350536

captcha