IQNA

Kiongozi wa Ansarullah Yemen

Yemen haitatoa muhanga uhuru wake

11:07 - October 14, 2015
Habari ID: 3385390
Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema watu wa nchi yake watailinda ardhi yao na hawatatoa muhanga 'heshima' na 'uhuru' mbele ya hujuma zisizo na kikomo za Saudi Arabia.

Akizungumza Jumapili katika mahojiano ya Televisheni, Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah Abdu-Malik al-Houthi amesema, "Leo kuna hujuma na njama za kuikalia kwa mabavu  nchi hii na kwa hivyo ni muhimu kwa Wayemen kutambua ukweli kuwa kuna wale ambao wanalenga kuidhibiti nchi hii."
Aidha amesema Marekani na Saudi Arabia ni chanzo cha masaibu ya watu wa eneo la Mashariki ya Kati. Ameongeza kuwa tawala za Israel na Saudia zinashirikiana katika mradi ya kuvuruga hali ya mambo katika eneo. Akiashiria kuendelea ukatili wa Saudia nchini Yemen amesema kuwa, 'kila mtu anapaswa kuelekea katika medani ya vita.'
Mapema Jumanne, Saudia ilitekeleza mashambulio 100 ya angani katika mkoa wa Sa'ada kaskazini magharibi mwa Yemen ambapo raia kadhaa walipoteza maisha wakiwemo wanawake na watoto.
Saudi Arabia imekuwa ikitekeleza mashambulizi kila siku dhidi ya Yemen tokea Machi 26 mwaka huu. Ripoti zinasema zaidi ya Waeyemen 6,400 wameuawa katika vita hivyo ambapo aghalabu ni raia hasa wanawake na watoto.../mh

3385268

captcha