IQNA

Muqawama

Kiongozi wa Ansarullah akosoa kimya mbele ya ‘Jinai ya Karne’

19:17 - August 16, 2024
Habari ID: 3479284
IQNA - Kiongozi wa harakati ya muqawama ya Ansarullah ya Yemen amelaani kuendelea kwa jinai za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Ghaza na ukimya na kutochukua hatua kwa baadhi ya nchi za Kiarabu.

Abdul-Malik al-Houthi amesema vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza kama "uhalifu wa karne".

Pia alisema majibu ya kambi ya Mhimili wa Muqawama kwa mauaji yaliyotekelezwa hivi karibuni na utawala wa Isarel huko Beirut na Tehran  ni "ya uhakika na yenye kuainisha hatima."

Al-Houthi amebaini kuwa kutumwa kwa meli za kivita za Marekani hakuwezi kuzuia vikosi vya Yemen kuanzisha operesheni ya kulipiza kisasi dhidi ya Israel baada ya shambulio lao kwenye mkoa wa kimkakati wa magharibi wa Hudaydah.

3489519

"Mrengo wa muqawama umedhamiria kabisa kulipiza kisasi dhidi ya mauaji yanayotekelezwa na Israel. Marekani inafanya kila iwezalo na kupitia njia za kisiasa ili kuzuia majibu ya vikundi vya muqawama dhidi ya mauaji yanayotekelezwa na Israel," alisema Alhamisi mchana.

“Majibu ya vitendo vya uchokozi vya utawala wa Kizayuni yanakaribia. Ni wajibu wa msingi wa imani, kibinadamu na kimaadili.”

Mkuu huyo wa Ansarullah amesema kulipiza kisasi dhidi ya utawala ghasibu wa Israel kutokana na mauaji ya shakhsia wa muqawama wa kieneo kumewafanya walowezi hao kuishi katika hali ya hofu kubwa.

Aidha amesema kulipiza kisasi dhidi ya adui wa Israel ni suala la kimkakati na ni la lazima kabisa ili kukomesha jinai zaidi za Israel.

Habari zinazohusiana
captcha