IQNA

Iran yakosoa sera za uharibifu za Saudia

15:27 - October 20, 2015
Habari ID: 3390838
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa sera za uharibifu za utawala wa Aal Saud na kusema kuwa hatua ya utawala huo ya kuishambulia nchi jirani yake ni ya kichokozi na yenye kudhihirisha uistikbari wa utawala huo.

Marzieh Afkham amesema ni jambo la kusikitisha sana kuona utawala huo unaendeleza mashambulizi dhidi ya Yemen licha ya juhudi za Iran na jamii ya kimataifa kulaani jinai hizo na kusisitiza udharura wa kusitishwa hujuma hizo. Kauli ya Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Iran ni radiamali kwa matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Adel al-Jubeir, ambaye alidai kuwa Tehran inaingilia mambo ya ndani ya Yemen.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa, tangu kuanza mashambulizi ya anga ya Saudi Arabia na waitifaki wake dhidi ya wananchi wa Yemen mwezi Machi mwaka huu, watu zaidi ya 5,000 wameuawa na wengine zaidi ya 25,000 kujeruhiwa.

3390711

Kishikizo: afkham saudia iran saud
captcha