
Maandamano hayo yamefanywa katika mkoa wa mashariki wa 
Qatif, ambapo waandamanaji walikuwa wakipiga nara za "Mauti kwa 
Aal-Saud" wakilaani mauaji ya kikatili ya msomi na mwanaharakati huyo wa
 Kiislamu. Baadhi ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na waandamanaji hao 
yalikuwa na ujumbe unaosema kuwa "Mikono ya serikali ya Riyadh imejaa 
damu ya watu wasio na hatia". Maandamano hayo yamefanyika siku moja 
baada ya familia ya Sheikh Nimr kuutaka utawala dhalimu wa Saudia kuikabidhi 
mwili wa mpendwa wao kwa ajili ya mazishi. Utawala wa Aal Saud tarehe Pili 
Januari mwaka huu ulimuua msomi huyo mkubwa wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia, hatua 
iliyokabiliwa na wimbi kubwa la malalamiko kutoka nchi mbalimbali 
hususan katika ulimwengu wa Kiislamu. Muhammad Nimr, mwana wa kiume wa 
msomi huyo hivi karibuni alinukuliwa akisema kuwa, utawala wa Aal Saud 
unafanya njama mbalimbali kuzusha fitna na migawanyiko kati ya Waislamu 
wa Kishia na Kisuni katika eneo hili na kuongeza kuwa watawala wa Saudia
 walimnyonga baba yake kutokana na misimamo yake ya kutetea haki za raia
 wa nchi hiyo, kinyume na madai yanayotolewa na baadhi ya duru kwamba 
Sheikh Nimr Baqir al Nimr alinyongwa kwa sababu ya hitilafu za kikabila. Waandamanaji halikadhalika walikuwa wamebeba bendera za Bahrain kama njia ya kuoneysha kufungamana na watu wa nchi hiyo ambao wanaadhimisha mwaka wa tano wa kuanza mwamko wa Kiislamu dhidi ya utawala wa kiimla wa Aal Khalifa nchini humo.
3474935