IQNA

Profesa Abdulaziz Sachedina: Ujumbe wa Imam Khomeini (RA) Uliotokana na Qur’ani

16:35 - December 05, 2025
Habari ID: 3481617
IQNA – Katika mahojiano ya mwaka 2015, Profesa Abdulaziz Sachedina, aliyewahi kufundisha masomo ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha George Mason, Virginia, Marekani, alisema kuwa ujumbe wa Imam Khomeini (RA), uliotokana na Qur’ani Tukufu, ulikuwa wa kiulimwengu na uliwahusu Waislamu wote.

Profesa Sachedina, msomi mashuhuri katika masomo ya kulinganisha ya Kiislamu, teolojia ya madhehebu ya Kiislamu ya Shia, na haki za binadamu, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 83 mjini Virginia, Jumatano.

Alitambulika kama mmoja wa wasomi wenye ushawishi mkubwa katika zama za sasa za Uislamu. Alizaliwa mwaka 1942 katika familia ya Kishia yenye asili ya Kihindi huko Tanzania, Afrika Mashariki, na kupata elimu ya awali huko. Malezi yake ya kitamaduni na kidini yaliweka msingi wa maswali ya utambulisho, uvumilivu na mazungumzo ya kidini, masuala yaliyomshughulisha katika maisha yake yote ya kielimu.

Akiwa kijana, alihamia India kusomea sayansi za jamii katika Chuo Kikuu cha Aligarh Muslim. Baadaye alisafiri Iran kuimarisha uelewa wake wa Ushia, akisomea katika Hawzah na Chuo Kikuu cha, Mashhad. Hapo ndipo jitihada zake za kuunganisha tafsiri ya maandiko na mbinu za kitaaluma zilipoanza kuchukua sura.

Hatua muhimu katika safari yake ya kielimu ilikuja alipohamia Kanada, alipata shahada ya uzamili na uzamivu katika Chuo Kikuu cha Toronto. Tasnifu yake ya PhD kuhusu maendeleo ya Mahdism katika Ushia wa Imamiya baadaye ikawa msingi wa kitabu chake mashuhuri 'Islamic Messianism'.

Kuanzia miaka ya 1970, alianza kufundisha katika Chuo Kikuu cha Virginia kwa zaidi ya miongo mitatu, kisha akajiunga na Chuo Kikuu cha George Mason y akiwa Mwenyekiti wa IIIT katika masomo ya Kiislamu. Mafundisho yake yalihusu teolojia ya Kiislamu (Shia na Sunni), historia ya fikra za Kiislamu, maadili ya kibiolojia  ya Kiislamu, Uislamu na haki za binadamu, pamoja na tafsiri za kulinganisha za Qur’ani.

Zaidi ya kufundisha, alihusika katika ujenzi wa taasisi za kielimu, mazungumzo ya kidini na kamati za maadili ya kitabibu. Miongoni mwa machapisho yake mashuhuri ni Islamic Messianism: The Idea of Mahdi in Twelver Shi‘ism, The Just Ruler in Shi‘ite Islam, Islamic Biomedical Ethics, Islamic Roots of Democratic Pluralism, na Islam and the Challenge of Human Rights.

Katika mahojiano na IQNA mwaka 2015, alipokuwa akihudhuria mkutano wa kimataifa mjini Tehran kuhusu Qur’ani Tukufu katika Maisha na Fikra za Imam Khomeini (RA), alisema:

“Ujumbe wa Imam Khomeini, uliotokana na Qur’ani, ni wa kiulimwengu na unawahusu Waislamu wote duniani. Qur’ani ni chanzo cha msukumo, na ujumbe wa Imam unaweza kusikilizwa na yeyote anayetafuta maana ya kiroho ya uwepo wa binadamu.”

Sachedina aliongeza:

“Imam alitufundisha kumtazama binadamu kama kiini cha uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Binadamu ndiye khalifa wa Mungu duniani na roho ya Mungu imo ndani yake.”

Akinukuu aya ya 70 ya Surah Al-Isra, alisema:

“Mwenyezi Mungu amewapa heshima na hadhi wanadamu wote bila kujali jinsia, rangi, kabila au imani. Neno Adam katika Qur’ani linawakilisha jina la pamoja kwa mwanadamu. Hii ndiyo roho ya Qur’ani ambayo pia imo katika ujumbe wa Imam Khomeini (RA).”

3495621

captcha