
Mashindano hayo, yajulikanayo kama “Pusti Verses of Light”, yanatarajiwa kufanyika katika Mwezi wa Ramadhani ya mwaka huu wa 1447 sawa na 2026.
Tangazo hilo lilitolewa Jumapili katika mkutano na wanahabari na Mohammad Mofassel Haque, mkurugenzi wa biashara wa TK Group.
Alisema kuwa lengo la mashindano haya ni kuwatambua na kuwaangazia wavulana na wasichana wenye vipaji vya kuhifadhi Qur’ani kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, na kuwapa jukwaa la kitaifa. Aliongeza kuwa mpango huu utaendelea kama sehemu ya juhudi za kuimarisha mazoea ya Qur’ani miongoni mwa vijana.
Sheikh Ahmad bin Yusuf Al‑Azhari, Qari mashuhuri kimataifa na mkuu wa majaji wa mashindano hayo, alisema kuwa hatua hii inawatia moyo watoto na vijana kuzidisha ukaribu wao na Qur’ani Tukufu. Pia alisifu TK Group kwa kuendeleza maadili ya Kiislamu kupitia programu hii.
Vijana Mahafidh kutoka maeneo mbalimbali ya Bangladesh watashiriki katika hatua za awali za kusailiwa, kisha majaji pamoja na wanazuoni wa Kiislamu watachagua washiriki watakaofuzu kuingia katika mashindano makuu.
Washindi watatunukiwa zawadi za fedha zinazofikia mamia ya maelfu, pamoja na tuzo nyingine.
Mchujo wa kitaifa utaanza Desemba 22, 2025.
Vipindi vikuu vya mashindano vitatangazwa kila siku katika mwezi wa Ramadhani, kuanzia saa 11 jioni hadi kabla ya adhana ya Maghribi, kupitia Channel Nine.
3495734