IQNA

Uwanja wa Bibi Fatima Zahra (SA) katika Haram ya Imam Ali (AS) wazinduliwa

16:55 - December 17, 2025
Habari ID: 3481671
IQNA – Baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Hazrat Zahra (SA) katika haram ya Imam Ali (AS), uwanja huo unazinduliwa leo.

Baada ya miaka 14 ya juhudi za wahandisi na wasanii wa Iran, pamoja na mchango na ushiriki wa wapenzi na waumini wa Imam Ali (AS), mradi wa Uwanja wa Hazrat Zahra (SA) ulio jirani na haram hiyo katika mji mtukufu wa Najaf Ashraf, ambao pia unatajwa kuwa mradi mkubwa zaidi wa upanuzi wa haram hiyo, unazinduliwa rasmi tarehe 17 Desemba.

Sehemu mbalimbali za uwanja huu zilikuwa tayari zimefunguliwa hatua kwa hatua katika miaka ya karibuni na kutumiwa na mahujaji wa haram hiyo, hususan wale wanaoshiriki matembezi ya Arbaeen.

Hata hivyo, ni sasa tu ambapo sehemu zote za mradi huo, ikiwemo makumbusho, maktaba, nyumba ya wahitaji, kitengo cha utawala na maegesho, zimekamilika kikamilifu.

Ujenzi wa uwanja huu ulifanyika chini ya usimamizi na juhudi za shahidi Jenerali Qassem Soleimani, kwa mchango wa wapenzi wa Ahlul-Bayt (AS) kutoka duniani kote, hasa wananchi wa Iran, na kwa kazi ya wahandisi na wasanii wa Iran kwa kipindi cha miaka 14 tangu 2011.

Jina “Uwanja wa Hadhrat Zahra (SA)” lilichaguliwa kwa pendekezo la Jenerali Soleimani na kwa idhini ya Marjaa Mkuu, Ayatullah Ali al-Sistani.

Uwanja huo umejengwa katika eneo la takribani mita za mraba 60,000 (urefu mita 400 na upana mita 150).

3495766

captcha