IQNA

Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani kufanyika Mauritania

11:15 - March 02, 2016
Habari ID: 3470175
Jumuiya ya wasoma Qur'ani Mauritania wamepanga kuandaa mashindano ya kitaifa ya Qur'ani nchini humo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wale ambao wanapanga kushiriki katika mashindano hayo wametakiwa kujisajili katika mashindano hayo yatakayofanyika katika mji mkuu, Nouakchott. Mashindano hayo yaliyopewa jina la al-Nour yatafanyika katika kategoria za kuhifadhi Qur'ani kikamiliofu na Tajweed.

Mashindano yatafanyika katika Masjid Ridhwan na kutangazwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya Qur'ani nchini humo.

Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritani ni nchi iliyo katika eneo la Maghreb huko kaskazini magharibi mwa Afrika. Karibu watu wote milioni 4 nchini humo ni Waislamu.

Harakati za Qur'ani hasa qiraa na hifdh ya Qur'ani Tukufu ni mashuhuri Mauritani hususan miongoni mwa vijana.

3479673

captcha