IQNA

19:52 - May 26, 2018
News ID: 3471532
TEHRAN (IQNA)- Duru ya 7 ya Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani maalumu kwa walemavu yamepangwa kufanyika Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuanzia Mei 27-31.

Kwa mujibu wa taarifa, Kituo cha Walemavu Dubai kimeandaa masshindano hayo ambayo yanatazamiw akuwa na washiriki 285 wa kike na kiume kutoka maeneo mbali mbali ya nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi.

Mashindano ya mwaka huu yameshuhudia ongezeko la asilimia 20 la washiriki ikilinganishwa na mwaka jana.

Mashindano hayo yatakuwa na kategoria za kuhifadhi Qur'ani kikamilifu, kuhifadhi juzuu 20,15,7,5,3, na mbili pamoja na kuhifadhi Juzuu moja au sura fupi fupi za Qur'ani.

Mbali na raia wa UAE, raia wa kigeni wanaoishi nchini humo pia wanatazamiwa kushiriki katika mashindano hayo.

3717442

Name:
Email:
* Comment: