IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya watoto walemavu

12:32 - February 13, 2019
Habari ID: 3471839
TEHRAN (IQNA) – Washindi wa Mashindano ya Qur'ani ya watoto walemavu yamefanyika nchini Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa taarifa Duru ya 23 ya Mashindano ya Kuhifadhi Qur'ani ya Sultan bin Salman yamefanyika Saudia katika makao makuu ya Jumuiya ya Watoto Walemavu.

Mashindano hayo yalijumuisha washiriki 2,384 kutoka nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi ambapo washindi walitunukiwa zawadi hivi karibuni katika sherehe zilizohudhuriwa pia na wazazi wao.

Majida Baysar, mwanachama wa Bodi ya Jumuiya ya Watoto Walemavu Saudia amewashukuru watoto walioshiri kwa kuonyesha nyuso zenye tabasamu na matumani huku akiwashukuru wazazi na waalimu kwa kuwapa washirki motisha, fikra chanya na matumaini ya kuwa wanadamu wenye manufaa kwa jamii.

3467915

captcha