IQNA

17:24 - June 16, 2019
News ID: 3472003
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Muungano wa Wasomaji na Waliohifadhi Qur'ani nchini Indonesia amesema hivi sasa kuna vituo 23,000 vya kufunza Qur'ani katika nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Asia.

Katika mahojiano maalumu na IQNA, Sayyid Aqil al-Munawwar ameongeza kuwa vituo hivyo vinaungwa mkono na kusimamiwa katika manispaa za miji ya nchi hiyo.

Ameongeza kuwa manpisaa huwa na nafasi muhimu sana katika ustawi wa elimu ya Qur'ani kote Indonesia.  Aidha amesema vituo hivyo vya Qur'ani vinafungamana na Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Indonesia.

Akijibu swali kuhusu viwango vya mafundisho ya Qur'ani na kidini katika vyuo vikuu vya Indonesia, Sayyid al-Munawwar amesema wanafunzi wa vyuo vikuu, hasa wale wanaosoma masoma ya Kiislamu, kwa kawaida huwa na kiwango kizuri cha kusoma na kuhifadhi Qur'ani huku baadhi pia wakiwa wamebobea katika tafsiri ya Qur'ani na Hadithi.

Sayyid al-Munawwar pia amegusia kuhusu mashundani ya Qur'ani nchini Indonesia na kusema kila mwaka hufanyika mashindano ya kitaifa ya Qur'ani na Sunna. Kuhusu mashindano ya kimataifa, amesema Indonesia iliandaa mashindano ya kimataifa kwa mara ya kwanza mwaka 2003 lakini baada ya miaka minne hayakuweza kuendelea. Hatahivyo amesema mashindano hayo yanatazamiwa kuanza tena baadaye mwaka huu.

Kwingineko, Sayyid al-Munawwar amesema wasomaji na waliohifadhi Qur'ani wanaweza kuwa na nafasi muhimu katika kuleta umoja na mshikamano katika jamii.

Sayyid Aqil al-Munawwar alizaliwa mwaka 1954 mjini Palembang, katika mkoa wa Sumatra kusini mwa Indonesia. Aliendeleza masomo yake ya juu na kuhitimu katika Chuo Kikuu cha Ummul Quraa cha Makka, Saudi Arabia. Aidha Sayyid al-Munawwar  ni qarii mashuhuri wa Qur'ani na hufunza Qur'ani na sayansi za Kiislamu katika vyuo vikuu nchini humo na aliwahi kuwa waziri wa masuala ya kidini nchini Indonesia kutoka mwaka 2001 hadi 2004 na

Sayyid al-Munawwar  amewahi kuwa jaji katika mashindano mengi ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu yakiwemo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

3818865

 
شهرداری‌های اندونزی جایگاه تأثیرگذاری در آموزش قرآن دارند
 
شهرداری‌های اندونزی جایگاه تأثیرگذاری در آموزش قرآن دارند
 
شهرداری‌های اندونزی جایگاه تأثیرگذاری در آموزش قرآن دارند
 
شهرداری‌های اندونزی جایگاه تأثیرگذاری در آموزش قرآن دارند
 
اندونزی
Name:
Email:
* Comment: