IQNA

16:02 - December 24, 2019
News ID: 3472299
TEHRAN (IQNA) – Pamoja na kuwa mustakabali wa uchumi wa Uingereza haujulikani kutokana na uamuzi wa nchi hiyo kujiondoa katika Umoja wa Ulaya, lakini biashara ya chakula halali nchini humo inazidi kuimarika kutokana kuongezeka matumizi miongoni mwa Waislamu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, miaka 10 iliyopita, nyama halali ilikuwa inapatikana tu katika bucheri zilizo katika maeneo yenye Waislamu wengi lakini hivi sasa Waislamu wana machaguo mengi sana ya kununua nyama au chakula halali.

Katika aghalabu ya supamaketi kubwa kote Uingereza kuna nyama halali zinazouzwa na pia chakula halali kilichopikwa.

Sekta ya bidhaa halali imestawi kwa kasi kubwa katika kipindi cha muongo moja uliopita. Katika soko la dunia, sekta halali inakadiriwa yenye thamani ya dola trilioni 3.6 huku nchini Uingereza sekta hiyo ikikadiriwa kuwa yenye thamani ya pauni bilioni moja. 

Kwa mujibu wa Nadeem Adam, Mkuu wa Oparesheni katika Kamati ya Kudhibiti Bidhaa na Chakula Halali Uingereza, ongezeko la hitajio la nyama halali linatokana na ongezeko la Waislamu nchini humo. Waislamu ni karibu asilimia nne ya watu wote Uingereza na hutumia asilimia 20 ya nyama yote inayozalishwa nchini humo.  

3470173

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: