Ayatullah Ibrahim Amini, mwanachama wa Baraza la Wanazuoni Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu aliaga dunia Ijumaa usiku mjini Qum baada ya kuugua kwa miezi kadhaa.
Katika ujumbe wake leo Jumamosi kufuatia kuaga dunia Ayatullah Amini, Ayatullah Khamenei ametuma salamu za rambi kwa chuo cha kidini cha Qum, wanafunzi na wapenzi wa mwanazuoni huyo mujahidi na kusema: "Umri uliojaa baraka wa mwanazuoni huyu mkubwa ulikuwa katika njia ya elimu, kutafuta na kusambaza maarifa ya Kiislamu na pia jihadi ya kisiasa na kijamii."
Aidha amesema mwanazuoni huyo mwendazake alishika nyadhifa rasmi katika mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu kama vile kuwa Imamu wa Swala ya Ijumaa na kuwa mwanachama wa Baraza la Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa hulka ya Ayatullah Amini ni mfano wa ucha Mungu na kutovutiwa na masuala ya kimaada na kidunia.