IQNA

Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajioun
12:50 - April 25, 2020
Habari ID: 3472700
TEHRAN (IQNA)- Ayatullah Ibrahimi Amini mwanazuoni maarufu, mwakilishi wa watu wa Tehran katika Baraza la Wanazuoni Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu na mwanachama wa Baraza la Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu Iran ameaga dunia na kurejea kwa Mola wake baada ya kuugua kwa muda.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Ayatullah Amini ameaga dunia Ijumaa akiwa na umri wa miaka 94 katika usiku wa kwanza wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka 1441 Hijria Qamaria. Ameaga dunia akiwa anapata matibabu katika Hospitali ya Shahid Beheshti mjini Qum.

Ayatullah Amini alizaliwa Juni 1925 katika mji wa Najaf Abad, mkoani Isfahan kati mwa Iran na alianza kuvutiwa na masomo ya dini akiwa bado ni mototo mdogo  mdogo. Aliweza kupata masomo kutoka kwa wanazuoni wakubwa wa zama zake kama vile Ayatullah Golpaygani, Ayatullah Maraashi Najafi, Imam Khomeini na Allamah Tabatabai – Mwenyezi Mungu Awarehemu-.

Alijiunga na harakati ya Imam Khomeini za kuupinga utawala wa kiimla wa Shah na baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979 alishikilia nyadhifa mbali mbali nchini Iran. Mwanazuoni mtajika huyo ameandika vitabu vingi kama vile ‘Uislamu na Malezi’, ‘Saumu, Zoezi la Wacha Mungu’ na ‘Ujue Uislamu’.

3893817

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: