IQNA

Polisi Norway wachunguza hujuma dhidi ya msikiti Norwich, Uingereza

22:33 - July 27, 2020
Habari ID: 3473004
TEHRAN (IQNA) – Polisi nchini Uingereza wanafanya uchunguzi baada ya msikiti kuhujumiwa nchini Uingereza katika mji wa Norwich.

Siju ya Jumtatu wazimamoto walipambana na moto saa saba usiku katika msikiti unaokarabatiwa kwa gharama ya Pauni milioni moja.

Polisi wamesema uchunguzi umebaini kuwa moto huo uliwashwa kwa makusudi  na kwamba wamebaini kuna mtu alifika hapo na kuwasha moto kabla ya kutoroka.

Jengo la msikiti huo zamani lilikuwa ni baa kabla ya Waislamu kulinunua na kuligeuza kuwa msikiti na ukarabati ungali unaendelea.

Msikiti huo unamilikiwa na Kituo cha Kiislamu cha East Anglian na unatazamiwa kuhudumia wakazi wa eneo hilo wanaozidi kuongezeka.

3472107

Kishikizo: norwich ، msikiti ، uingereza
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha