IQNA

Swala ya Ijumaa yaanza tena nchini Uganda

21:38 - September 26, 2020
Habari ID: 3473204
TEHRAN (IQNA) - Sala za Ijumaa zimeanza tena nchini Uganda baada ya kusimamishwa kwa muda wa takribani miezi sita kutokana na maambukizi ya kirusi cha corona.

Mufti wa Uganda Sheikh Ramadhan Mubajje aliongoza Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Kitaifa eneo la Old Kampala.

Amesema serikali itatumia kipindi hiki cha kupunguzwa utekelezwaji wa kanuni za kuzuia corona kuona ni vipi nyumba za ibada zitazingatia kanuni za kiaffya zilizowekwa. Sheikh Mubajje ametoa wito kwa Waislamu kuzingatia maelezo ya serikali kuhusiana na kukabiliana na corona. Naye Mufti Mkuu wa Uganda Sheikh Silimani Ndirangwa ametoa wito kwa serikali kuondoa marufu ya swala za jamaa.

Hadi sasa watu 7,218 wameambukizwa corona nchini Uganda ambapo waliofariki ni 71.

3925337

captcha