IQNA

Fikra za Kiislamu

Barzakh iko wapi?

20:24 - October 01, 2022
Habari ID: 3475865
TEHRAN (IQNA) – Katika imani ya Kiislamu, Barzakh ni jukwaa baina ya dunia na akhera ambalo linatutayarisha kutoka kwenye hatua ya dunia hii tuliyopo hadi dunia ijayo.

Katika itikadi ya Kikatoliki jukwaa ambalo kwa kiasi fulani linashabihiana na Barzakh linajulikana kama Toharani.

Kwa kuzingatia aya za Quran Tukufu na Hadithi, hali zetu katika Barzakh zitategemea jinsi tulivyoishi maisha yetu hapa duniani.

Barzakh kwa namna fulani ni muendelezo wa dunia hii na maisha ya mwanadamu baada ya kifo.

Ni kituo cha kwanza ambapo roho huenda baada ya kujibu maswali wakati roho ya mtu inatoka na kuwekwa kwenye kaburi lake. Kisha atakuwa katika Barzakh mpaka Siku ya Kiyama.

Barzakh ni ulimwengu wa muda na mahali pa kujitayarisha kwa ajili ya Siku ya Hukumu na kisha baada ya hapo ima mwanadamu ataelekea mbinguni au motoni.

Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, Barzakh ipo kwa ajili ya waumini na makafiri. Tofauti ni kwamba ni mahali pazuri na pa amani na utulivu kwa waumini na mahali pabaya na penye masaibu kwa makafiri. Wakiwa Barzakh, makafiri wanatafuta njia ya kurejea duniani na kurekebisha vitendo vyao lakini hilo haliwezekani.

Katika Qur’ani Tukufu tunasoma hivi.

“Mauti yanapomfikia mmoja wa makafiri, husema, ‘Mola wangu Mlezi! Nirudishe. Ili nitende mema sasa badala ya yale niliyo yaacha. Wapi! Hii ni kauli aisemayo yeye tu. Na nyuma yao kipo kizuizi mpaka siku watapo fufuliwa." (Surah Al-Muminun, Aya ya 99-100)

Katika Barzakh hakuna uwezekano kufanya matendo yanayoegemezwa kwenye hiari ingawa baadhi ya matendo tuliyokuwa nayo katika ulimwengu huu yanaweza kuendelea kuathiri hali yetu huko.

Maswali ya Malaika wawili Nakir na Munkar, udhihirisho wa imani na matendo tuliyokuwa nayo katika ulimwengu huu, na mwingiliano wa wale walio katika Barzakh baina yao na ulimwengu huu ni miongoni mwa sifa za Barzakh ambazo zimefafanuliwa katika Hadithi. Munkar na Nakir ni Malaika ambao huitembelea roho ili kuiuliza kuhusu dini yake baada ya kuaga dunia.

Lakini sifa muhimu zaidi ya Barzakh ni kwamba hakuna mtu, hata wanafamilia wetu na marafiki zetu, wanaweza kutusaidia huko.

 Basi kwa ajili ya makosa yao waligharikishwa wakaingizwa Motoni, wala hawakuwapata wa kuwanusuru badala ya Mwenyezi Mungu.” (Surah Nuh, Aya ya 25)

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha