IQNA

Fikra za Kiislamu

Mawazo mazuri husaidia mtu kupata njia sahihi

20:38 - October 01, 2022
Habari ID: 3475866
TEHRAN (IQNA) – Kuna msisitizo mkubwa ndani ya Qur’an Tukufu juu ya kufikiri na kutafakari kwa sababu kutafakari kunasaidia kumzuia mtu asipotee na kutafuta njia iliyo sawa.

Mwanadamu ameumbwa akiwa kiumbe mwenye mawazo na sifa muhimu zaidi inayomtofautisha na viumbe vingine ni uwezo wa kufikiri na kutafakari.

Hata hivyo, kufikiri kunaweza kusiwe chanya kila wakati. Baadhi ya fikra zisizo na manufaa zinaweza hata kusababisha mtu kukengeuka kutoka kwenye njia inayomfikisha kwenye malengo yake.

Kwa hivyo ni lazima mtu ajue na ayafahamu mawazo ambayeo humsaidia na kumpeleka kwenye mwongozo na kutafakari juu ya mawazo hayo.

Baadhi  ya aya za Qur’ani Tukufu Mungu zinaangazia masuala ambayo mtu anatakiwa kuyatafakari. Moja ya masuala haya ni ulimwengu wa uumbaji.

“Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala, na hufikiri kuumbwa mbingu na ardhi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuviumba hivi bure. Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya Moto.” (Sura Al-Imran, Aya ya 191).

Somo lingine ambalo ni vizuri kutafakari ni historia na hatima ya watu walioishi kabla yetu. Aya ya 21 ya Sura Ghafir inasema: “Kwani hawatembei katika ardhi wakaona jinsi ulivyo kuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao? Hao walikuwa wamewazidi hawa kwa nguvu na athari katika nchi. Na Mwenyezi Mungu aliwatia mkononi kwa sababu ya madhambi yao. Na wala hapakuwa wa kuwalinda na Mwenyezi Mungu.”

Kwa upande mwingine, kuna masuala ambayo tunashauriwa tusiyafikirie kwa sababu yatatuletea matatizo na madhara.

Kishikizo: fikra za kiislamu ، mawazo
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha