IQNA

Fikra za Kiislamu

Kujitolea: Njia ya Kufikia Wokovu

22:19 - October 08, 2022
Habari ID: 3475900
TEHRAN (IQNA) – Kila mwanadamu ana malengo matukufu maishani na anajitahidi kuyafikia kwa kutumia uwezo wake wote. Walakini, kuna nyakati maishani ambapo mtu anapendelea kutoa sehemu kubwa ya uwezo wake kwa wengine, na hii inajulikana kama kujitolea.

Kujitolea ina maana ya kupendelea wengine kuliko wewe mwenyewe na inajumuisha kuwapa wengine kile mtu anachohitaji yeye mwenyewe. Kutoa muhanga maisha ya mtu, mali, nafasi, nk, katika njia ya Mwenyezi Mungu ni aina ya kujitolea.

Ni kati ya ishara nzuri zaidi za ubinadamu. Qur'ani Tukufu imeashiria mifano ya kujitolea na kuisifu. Kwa mfano, Ansar walikuwa watu wa Madina ambao, licha ya mahitaji yao wenyewe, walitoa mali zao na nyumba kwa wale waliokuja kutoka Makka wakifuatana na Mtukufu Mtume (SAW).

"Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa. (Surah Al-Hashr, Aya ya 9)

Jambo muhimu zaidi katika kujitolea ni usafi wa nia na kuepuka unafiki na kuwafanya wengine wadhalilike kutokana na misaada waliopekea.

Kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu: Enyi mlio amini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na maudhi, kama anaye toa mali yake kwa kuwaonyesha watu, wala hamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama mfano wa jabali ambalo juu yake pana udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa, ikaliacha tupu. Basi hawatakuwa na uweza wowote kwa walivyo chuma. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri.” (Surah Al-Baqarah, Aya ya 264)

captcha