IQNA

Fikra za Kiislamu

Mtazamo wa Qur'ani Tukufu kuhusu madhumuni ya uumbaji

18:55 - October 05, 2022
Habari ID: 3475885
TEHRAN (IQNA) – Qur’ani Tukufu ni kitabu cha maisha kinachowaongoza wanadamu kwenye ukamilifu na ufanisi; kwa hivyo inategemewa kwamba Kitabu hiki kitatoa majibu kwa maswali ya kimsingi kuhusu maisha.

Moja ya maswali muhimu kwa watu binafsi imekuwa falsafa ya uumbaji. Siku zote wanadamu wametafuta kuelewa kusudi la kuumbwa na uhai wao.

Baadhi ya aya za Qur'ani zinataja majaribio au mitihani anayopata mwandamu kuwa moja kati ya madhumuni ya uumbaji. “Na Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Na Kiti chake cha Enzi kilikuwa juu ya maji, ili akufanyieni mtihani ajuulikane ni nani miongoni mwenu mzuri zaidi wa vitendo. Na wewe ukisema: Nyinyi hakika mtafufuliwa baada ya kufa; wale walio kufuru husema: Hayakuwa haya ila ni uchawi uliyo wazi.” (Sura Hud, aya ya 7)

Au katika aya ya 2 ya Surah Al-Mulk isemayo: “ Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha. 

Aya hizi mbili zinataja mitihani na majaribio kama lengo la uumbaji. Vile vile Mwenyezi Mungu Mtukufu ameumba baraka katika ardhi kwa ajili ya kuwajaribu wanadamu: “Kwa hakika tumevifanya vilioko juu ya ardhi kuwa ni pambo lake ili tuwafanyie mtihani, ni nani kati yao wenye vitendo vizuri zaidi. " (Sura Al-Kahf, aya ya 7)

Majaribio na mitihani wakati mwingine huja kupitia misiba na wakati mwingine kupitia baraka na matukio mema. Kitendo cha Mungu kujaribu wanadamu ni cha kipekee kikilinganishwa na uhusiano wake na viumbe vingine.

Mitihani hii ni sehemu na chanzo cha mwanadamu kumuabudu Mwenyezi Mungu na huwa ni kigezo cha mwanadamu kupitia ngazi mbali mbali za kuwa mja mwema wa Mwenyezi Mungu. Vipimo vidogo huwafanya watu kuwa tayari kwa magumu zaidi katika hatua za juu zaidi.

Kwa msingi huo mitihani na majaribio huwa njia ya mwanadamu kufikia ukamilifu au ubora na umaanawi wa kiwango cha juu na kilichobora kabisa.

Kishikizo: uislamu ، ، madhumuni ، qurani tukufu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha