IQNA

Fikra za Kiislamu

Dhiki zinazoleta matumaini ya faraja

22:16 - September 30, 2022
Habari ID: 3475861
TEHRAN (IQNA) – Wakati wa uhai wake na katika safari yake hapa duniani, mwanadamu hukabiliana na matatizo na dhiki mbalimbali.

Wanafikra wengi wametafakari na kuzungumzia sababu inayowafanya wanadamu kuteseka. Kulingana na sheria za Kimungu, shida huleta faraja na utulivu.

Mwenyezi Mungu amemuumba mwanadamu kukabiliana na dhiki na matatizo: “Hakika Sisi tumemuumba mtu katika taabu na mapambano. (Surah Al-Balad, Aya ya 4)

Shida hizi ni za kufundisha na kusaidia talanta na uwezo wa mtu kustawi.

Kwa hakika, ukamilifu na maendeleo mengi hayawezi kupatikana bila kukabili matatizo na mapambano.

Pia, sifa nyingi nzuri kama vile subira, ushupavu, Ridha (kuridhika na Mungu), Zuhd (uchamungu), Taqwa (kumcha Mungu), na kujitolea mhanga, huundwa wakati wa kukabili matatizo.

Kwa kuongezea, baadhi ya mateso na shida ni matokeo ya dhambi au makosa ambayo mtu hufanya. Matatizo humkumba mwanadamu ili atambue hatua zake mbaya na kujaribu kuzirekebisha.

Ni adhabu za Mwenyezi Mungu ambazo zinalenga kutusaidia kupata njia sahihi na kurudi kutoka kwenye njia ya upotofu na ujinga.

Vyovyote iwavyo, ikiwa magumu yanajaribu imani yetu na kutusaidia kukua au ni adhabu kwa ajili ya makosa yetu, tunaweza kupata utulivu na kuyapitia kwa kumuomba Mwenyezi Mungu na kuwa na Tawakkul (kumtegemea Mungu) kwa sababu kutakuwa na wepesi baada ya kila dhiki. .

“Hakika baada ya kila shida kuna nafuu.” (Surat Ash-Sharh, Aya ya 5)

Mungu ametupa uwezo wa kuyakabili magumu na ni juu yetu kuyatumia kuyapita na kufikia raha na amani.

Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 155 ya Surah Al-Baqarah: “Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri,”

Mwenyezi Mungu, ambaye ni mwingi wa huruma na mwingi wa rehema, ameumba magumu kwa ajili ya ukamilifu wa nafsi ya mwanadamu.

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha