IQNA

Mawaidha

Eneo la baina ya Dunia na Siku ya Kiyama

22:07 - November 13, 2024
Habari ID: 3479748
IQNA – Neno Barzakh maana yake ni eneo au hali ya baina ya vitu viwili. Hivyo basi, Barzakh (toharani) ni jukwaa baina ya dunia na Siku ya Kiyama.

Katika imani ya Kiislamu, Barzakh ni jukwaa baina ya dunia na akhera ambalo linatutayarisha kutoka kwenye hatua ya dunia hii tuliyopo hadi dunia ijayo.
Katika itikadi ya Kikatoliki jukwaa ambalo kwa kiasi fulani linashabihiana na Barzakh linajulikana kama Toharani.
Kuna aya nyingi ndani ya Qur'an Tukufu zinazotaja Barzakh, wakati mwingine huiita "ulimwengu wa kaburi" na wakati mwingine "ulimwengu wa roho".
Aya moja kama hiyo ni Aya ya 100 ya Surah Al-Muminoon: “Ili nitende mema sasa badala ya yale niliyo yaacha. Wapi! Hii ni kauli aisemayo yeye tu. Na nyuma yao kipo kizuizi mpaka siku watapo fufuliwa.”
Aya nyingine zinazothibitisha kwa uwazi kuwepo kwa Barzakh ni zile zinazohusu mashahidi.

Aya nyingine zinazothibitisha kwa uwazi kabisa kuwepo kwa Barzakh ni zile zinazohusu mashahidi, kama vile Aya ya 169 ya Surah Al Imran ambamo Mwenyezi Mungu anamwambia Mtukufu Mtume (SAW.): “Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi.”

Katika Aya ya 154 ya Surah Al-Baqarah, Mwenyezi Mungu anawaambia waumini wote: “Wala msiseme kuwa wale walio uwawa katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni maiti; bali hao ni wahai, lakini nyinyi hamtambui.”
Barzakh haipo tu kwa wale walio na hadhi ya juu, kama vile mashahidi, bali pia kwa makafiri waasi, kama vile Firauni na masahaba zake.
Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 46 ya Surat Al-Ghafir: “Wanaonyeshwa Moto asubuhi na jioni. Na itapo fika Saa ya Kiyama patasemwa: Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!”
Isisahaulike kwamba akhera ni tofauti na Barzakh. Akhera ina maana pana na inahusu ulimwengu baada ya dunia hii. Inajumuisha Barzakh, Siku ya Kiyama na baadaye. Kwa hiyo Barzakh ni sehemu ya maisha ya baada ya kifo ambapo watu huwekwa baada kifo hadi Siku ya Hukumu au Siku ya Kiyama.

Kishikizo: qurani tukufu barzakh
captcha