IQNA

Miujiza ya Nabii Isa (AS) katika Qur’ani Tukufu

18:40 - June 26, 2023
Habari ID: 3477195
Nabii Isa (AS) alikuwa miongoni mwa Ulul Azm (watano wakubwa) mitume wa Mwenyezi Mungu na Qur'ani Tukufu inazingatia sana tabia yake.

 

Quran Tukufu  inaangazia miujiza ya Nabii Issa (AS), ambayo ilikusudiwa kuwasaidia watu kuamini.

Nabii Isa (AS) alikuwa na miujiza mingi ambayo ilikuwa ni dalili za utume wake na uhusiano wake na Mwenyezi Mungu ili watu wasadikike kwamba hakika yeye ni nabii wa Mwenyezi  Mungu.

Muujiza wa kwanza wa  Nabii Isaa ulikuwa kuzaliwa kwake, Kwa mujibu wa Quran Tukufu Bi Maryam  (SA) alibeba  mimba bila ya kuolewa au kuwa na mahusiano yoyote na mwanamume, Kwa mujibu wa Quran Tukufu  kuzaliwa kwake kwa njia hii ilikuwa ni ishara kwa watu na rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Akasema; Hili ni kweli lakini Mola wenu Mlezi anasema;  Ni mepesi sana kwangu tumeamua kukupa mtoto  awe ni ushahidi wa kuwepo kwetu kwa wanadamu na rehema kutoka kwetu, Hili ni agizo lililokwisha wekwa, Tafsiri ya  Aya ya 21 ya Surati  Maryam.

Muujiza wa pili wa  ulikuwa kuzungumza katika utoto yani akiwa mtoto Akasema mtoto; ‘Mimi ni mfuasi  wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu amenipa Kitabu na amenifanya Nabii, Tafsiri ya  Aya ya 30 ya Surati  Maryam.

Pia alikuwa na miujiza wakati wa utume wake wa kinabii, Kwa mfano, Tafsiri ya  aya ya 49 ya Surati Al Imran inaashiria miujiza yake minne, nayo ni kutengeneza ndege halisi kwa udongo, kumponya kipofu aliyezaliwa kipofu, kufufua wafu, na kuwaambia watu juu ya yale yaliyofichika, Atakuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa Wana wa Israili ambaye atawaambia.

  Nimekuleteeni muujiza kutoka kwa Mola wenu Mlezi, Mimi ninaweza kukuumbieni udongo katika umbo la ndege, Nikipuliza ndani yake, huwa atakuwa ndege wa kweli, kwa idhini ya Mungu,Naweza kuwaponya vipofu na wenye ukoma na kuwafufua wafu, kwa idhini ya  Mwenyezi Mungu, naweza kuwaambia mnachokula na mnachoweka akiba katika nyumba zenu. Huu ni muujiza kwenu kama mnataka kuwa na imani.

Muujiza mwingine wa Nabii Issa ulikuwa ni kumwomba mwenyezi  Mungu ateremshie chakula kutoka mbinguni, Wanafunzi waliposema, ‘Ewe (Nabii) Issa, mtoto  wa Maryamu, je, Mola wako anaweza kututeremshia meza kutoka mbinguni? Tafsiri ya  Aya ya 112 ya Surati  Al-Maidah.

Mwenyezi Mungu kasema; ‘Mimi ninakuleteeni, lakini yeyote miongoni mwenu akigeuka na kuwa makafiri, nitamtia adhabu ambayo hajawahi kuipata yeyote Tafsiri ya  Aya ya 115 ya Surati Al-Ma’idah.

 

3484084

 

Kishikizo: miujiza ya isa
captcha