Inasadifiana na kukamilika kwa Hija - hija tukufu ya Makka - huko Saudi Arabia, ambayo ni wajibu kwa kila Mwislamu mwenye uwezo mara moja katika maisha yao.
Inaangukia siku ya 10 ya Dhul Hijjah, mwezi wa mwisho na mtakatifu zaidi wa kalenda ya mwandamo ya Kiislamu. Waislamu mara nyingi hufunga siku tisa za mwanzo wa mwezi huu kutafuta rehema na baraka za Mwenyezi Mungu.
Mwaka huu, nchi nyingi zitasherehekea Eid al-Adha siku ya Jumatano, wakati baadhi ya maeneo kama vile Pakistan na India zitaiadhimisha siku ya Alhamisi.
Tamasha hilo ni ukumbusho wa kisa cha Nabii Ibrahim, au Ibrahim, ambaye anaheshimiwa na Waislamu, Wakristo na Wayahudi kama baba wa tauhidi. Mungu alijaribu imani yake kwa kumwomba amtoe dhabihu mwanawe Ismail.
Nabii Ibrahim na Ismail walijisalimisha kwa hiari kwa amri ya Mwenyezi Mungu na kujitayarisha kwa ajili ya dhabihu kama kitendo cha kujitolea na utii. Ibilisi - anayejulikana kama "Iblis" katika Uislamu - alijaribu kuwajaribu mbali na mapenzi ya Mungu, lakini walimpiga mawe ili kumfukuza.
Kitendo hiki kinaigizwa tena na Waislamu kama ibada ya Hjja, ambapo wanarusha kokoto kwenye nguzo tatu zinazoashiria shetani katika mji wa Mina.
Nabii Ibrahim na Ismail (AS) walipokaribia kutoa dhabihu, Mwenyezi Mungu alimbadilisha Ismail na kuweka mwanakondoo kutoka mbinguni, kwa mujibu wa mapokeo ya Kiislamu, Toleo kama hilo la hadithi pia linapatikana katika Ukristo na Uyahudi.
Sadaka ni ishara ya kuacha tamaa za kidunia na kwa kufanya hivyo, waamini hujaribu kuimarisha uchamungu wao, kutubu dhambi zao, kujifunza kuweka maagizo ya kimungu kwanza na kumshinda Shetani.
Kutoa muhanga si desturi mpya ambayo Uislamu uliianzisha, lakini imefanywa na dini za awali pia, Hata hivyo, Uislamu una tofauti fulani katika jinsi unavyofanya ibada hii, Tofauti muhimu zaidi ni kwamba dhabihu ni kwa ajili ya Mungu Mwenyezi tu, si kwa ajili ya nyota, malaika, au watu, Uislamu hauruhusu kutoa kafara kwa ajili ya mtu yeyote au kitu kingine chochote.
Si mwili na damu ya dhabihu yako ndiyo inayompendeza Mwenezi Mungu, Kinachompendeza Mwenyezi Mungu ni uchaji wako, Surati Hja, aya ya 37.
Baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu wanasema kinachompendeza Mungu si kitendo tu cha kuua mnyama, bali ni kuwalisha wengine,Mwenyezi Mungu anataka watu binafsi wawe wakamilifu katika maisha yao ya kibinafsi na ya kijamii kwani kumwaga tu damu hakutawasaidia kufikia hilo.
Sababu nyingine ya dhabihu ni kwamba inawafundisha waaminifu kujitoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na njia yake, Kwa kufanya tendo hilo, wanajifunza kuwa tayari kutoa maisha au mali zao kwa ajili ya Mungu Mwenyezi.
Waislamu kote ulimwenguni husherehekea Eid al-Adha kuheshimu ibada na kujitolea kwa Nabii Ibrahim na Nabii Ismail (AS).
Moja ya mila kuu inayohusishwa na sikukuu ni dhabihu ya mfano ya mnyama, ambayo sio lazima lakini inapendekezwa sana katika Uislam,. Mnyama anapaswa kuwa na afya na kulishwa vizuri, na kuchinjwa kwake kunapaswa kufanywa kwa maumivu na mateso kidogo.
Nyama kutoka kwa mnyama yeyote aliyetolewa dhabihu hugawanywa kati ya maskini, pamoja na wanafamilia na marafiki. Kondoo, mbuzi au mwana-kondoo anaweza kutolewa dhabihu na mtu mmoja, wakati ng'ombe au ngamia wanaweza kugawanywa na watu saba.
Sadaka ni thamani ya msingi katika Uislamu, na Zakat, desturi ya Waislamu ya kutoa sadaka, ikiwa ni moja ya kanuni kuu, Eid al-Adha inawapa Waislamu fursa nyingine ya kuwasaidia wale wanaohitaji.
Waislamu wengi pia huchagua kuchangia thamani ya mnyama kwa mashirika ya misaada ambayo hutoa nyama kwa watu duniani kote, hasa katika maeneo ambayo njaa na umaskini umeenea zaidi.
Kinachotokea kufuatia dhabihu katika Hija.
Mamilioni ya Waislamu wanaohiji huchinja mnyama katika siku ya tatu ya Hijja.
Baada ya kafara, wanapunguza nywele zao au wananyoa vichwa vyao na kubadilisha kutoka kwenye ihram ya hujaji wao, nguo nyeupe zinazovaliwa mahsusi kwa ajili ya Hija ili kuashiria hali ya usafi na kujitenga na mambo ya kidunia, na kufuta tofauti za mali na hadhi miongoni mwao Waislamu.
Katika siku chache zijazo, wao hufanya tawaf, wakati mahujaji wanapozunguka Kaaba mara saba kinyume na saa, Kaaba ni muundo mweusi wenye umbo la mchemraba ambao Waislamu wanaichukulia kuwa nyumba ya Mungu iliyojengwa na Nabii Ibrahim na Ismail.
Pia wanarudia ibada inayojulikana kama sai, kutembea au kukimbia mara saba kati ya vilima vya Safa na Marwa, kabla ya kurudi kuzipiga mawe nguzo tatu zinazowakilisha shetani.
Hatimaye, wanafanya tawafu ya kuaga ili kukamilisha Hija yao kabla ya kuondoka Makka kuelekea nchi Mwao.