IQNA

Mufti Mkuu wa Oman ataka Israel ilazimishwe isitishe ukiukaji wa makubaliano ya Gaza

11:03 - November 17, 2025
Habari ID: 3481527
IQNA – Mufti Mkuu wa Oman ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa na nchi za Kiislamu kuushinikiza utawala wa Kizayuni kusitisha ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.

“Sheikh Ahmed bin Hamad Al Khalili alisema tunashangazwa na mwenendo wa utawala wa Kizayuni unaojaribu kupotosha makubaliano ya Gaza, yaliyofikiwa kwa uwepo wa baadhi ya nchi za Kiarabu na mataifa mengine,” aliandika katika ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, kwa mujibu wa taarifa ya Al-Mayadeen.

Aliongeza: “Tunaziomba jumuiya ya kimataifa kuishinikiza Israel isije ikakiuka ahadi zake katika makubaliano ya Gaza.”

Mufti Mkuu wa Oman pia amezitaka hasa nchi za Kiislamu na jamii zao kwa ujumla kusimama haraka kwa mshikamano na ndugu zao wa Gaza, ili adui asifanikiwe kutekeleza mipango yake ya kihalifu.

Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, na utawala wa Israel yalifikiwa tarehe 10 Oktoba.

Tangu wakati huo, Israel imekiuka makubaliano hayo mamia ya mara, na kusababisha vifo vya Wapalestina wengi. Aidha, utawala huo umezuia kwa makusudi kuwasilishwa kwa misaada ya kibinadamu inayohitajika kwa dharura.

4317100

Habari zinazohusiana
Kishikizo: israel mufti wa oman
captcha