IQNA

Wanafunzi wa Iran waanza safari ya Umrah kuelekea ardhi ya Wahyi

11:10 - November 17, 2025
Habari ID: 3481528
IQNA – Hafla ya kuaga kundi la kwanza la wanafunzi wanaoelekea katika ibada ya Hija ndogo ya Umrah kutoka vyuo vikuu imefanyika mjini Tehran Jumapili, katika kituo cha Salam cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Imam Khomeini.

Kwa mujibu wa Hujjatul Islam Seyed Mohammad Taheri, mkuu wa Makao ya Mahujaji wa Vyuo Vikuu, makundi ya kwanza ya wanafunzi yameondoka kutoka Tehran na Sari kuelekea Ardhi ya Ufunuo.

Amesema jumla ya wanafunzi na wahadhiri 8,000 wa vyuo vikuu watashiriki katika awamu ya 21 ya Umrah ya kitaaluma. Msafara wa mwisho utasafiri tarehe 18 Desemba na kurejea nyumbani tarehe 28 Desemba.

Akibainisha umuhimu wa vipindi vya kiutamaduni na kiroho vilivyopangwa kwa wanafunzi hao, Taheri alisema maandalizi maalum yamefanyika Makka na Madina nchini Saudi Arabia na ratiba mahsusi imeandaliwa kwa ajili ya misafara ya wanafunzi katika miji hiyo mitakatifu.

Aliongeza kuwa miongoni mwa vipindi hivyo ni usomaji wa Qur’ani Tukufu na dua, sambamba na mihadhara ya mawaidha na vipindi vya kielimu vitakavyotolewa na wahubiri na wasemaji waliyoalikwa, ili wanafunzi wapate manufaa ya kielimu na kiroho.

Umrah ni ibada ya Mustahab (inayopendekezwa lakini si ya lazima) ya kwenda Makka, ambayo Waislamu wanaweza kuitekeleza wakati wowote wa mwaka. Umrah ni tofauti na Hija ambayo ni faradhi kwa kila Muislamu mwenye uwezo wa kifedha na kiafya mara moja tu maishani, na hufanyika katika siku za mwanzo za mwezi wa Dhul-Hijja kwa mujibu wa kalenda ya Hijria.

4317169

Habari zinazohusiana
Kishikizo: umrah iran wanafunzi
captcha