Mungu anajua unachotaka, unachohitaji na unachoomba na kumwomba. Kwa hiyo, muombe Mungu. Mahali pengine anasema: "Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni." Bila shaka, jibu hili halimaanishi kujibuwa haja ulizonazo papo hapo, maana yake ni kuwa Mwenyezi Mungu amesikia na ameitikia. Anasema: "Najibu na nitakuitikieni"; Jibu hili la Mwenyezi Mungu pia mara nyingi, linaambatana na utoaji wa unalohitajia au jambo uliloomba. "
17/02/1995