IQNA

Hija

Kundi la kwanza la Wairani walioelekea Hija wawasili Madina

23:20 - May 13, 2024
Habari ID: 3478816
IQNA - Kundi la kwanza la Wairani walioelekea Hija kutoka Iran waliwasili katika mji mtakatifu wa Madina Jumatatu Mei 13.

Kundi hilo la kwanza lilijumuisha wauminii wapatao 250 kutoka mikoa ya Tehran na Kermanshah. Walikuwa wameondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Imam Khomeini (RA) wa Tehran mapema Jumatatu.

Mahujaji hao wa Iran walikaribishwa katika uwanja wa ndege wa Madina kwa maua na maji ya waridi na kisha kuelekea katika hoteli zao.
Safari za ndege zinazoondoka kwenda Saudi Arabia zitaendelea hadi Juni 2, ripoti hiyo ilibainisha, na kuongeza kuwa Wairani wataendelea kusalia Saudi Arabia kwa wastani wa siku 33. Kulingana na maafisa wa Hijja, Wairani 87,550 wamekamilisha usajili kwa ajili ya kushiriki katika safari ya kiroho ya Hija mwaka huu.
Wakati huo huo, Hujjat al-Islam Syed Abdul Fattah Nawab, mwakilishi wa Faqihi Mtawala katika masuala ya Hijja na Ziyara ambaye pia ni msimamizi wa Mahujaji wa Iran aliaga kundi hilo la kwanza la Wairani wanaolekea Hija mapema leo na kusema: "Kauli mbiu ya Hija ya mwaka huu ni "Uzingatiaji Qur'ani, Huruma na Nguvu za Kiislamu na Kutetea Palestina Inayodhulumiwa." Amewashauri wanaoelekea Hija kuwa, wanapotembelea Al Masjid An Nabawi (SAW ) na Masjid Al-Haram wajitahidi kuhitimisha qiraa ya Qur'ani Tukufu.

Msimamizi wa Mahujaji wa Iran aidha amesema nguvu na uwezo wa Kiislamu na Palestina inayodhulumiwa ni sehemu nyingine ya nara ya Hija ya mwaka huu. Ameongeza kuwa Mahujaji wanapaswa kufuata sira ya Manabii na kuwaombea ushindi wananchi wa Palestina wakiwa katika ardhi ya Wahyi.

Kila mwaka katika mwezi wa Dhul Hijjah, Saudi Arabia hukaribisha Waislamu wapatao milioni mbili wanaonuia kutekeleza ibada ya Hijja.

3488327

captcha