IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Vijana wanapaswa kuwa kitovu cha mazingatio ya ubunifu wa matangazo yanayotegemea mbinu za kisasa

16:08 - July 12, 2023
Habari ID: 3477273
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa kizazi cha vijana, wakiwa ndio wamiliki na viongozi wa kesho wa nchi, kinapaswa kuwa kitovu cha mazingatio ya ubunifu wa matangazo yanayotegemea mbinu na zana za kisasa.

Akizungumza leo Jumatano mbele ya hadhara ya wanazuoni, wanafunzi na wahubiri wa vyuo vya kidini katika kukaribia mwezi mtukufu wa Muharram, Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, ameeleza kuwa mahitaji ya nchi kwa shughuli za uhubiri na uenezaji zinazotegemea utafiti, ni makubwa zaidi kuliko shughuli hizo zilivyo hivi sasa. Huku akitolea hoja Aya kadhaa za Qur'ani Tukufu kuhusu mahubiri na taathira zake, Ayatullah Khamanei, amesema dini ya Mwenyezi Mungu haiwezi kuenezwa miongoni mwa umati wa watu isipokuwa kwa kutegemea njia sahihi za mahubiri.

Akiashiria umuhimu wa mila ya muda mrefu ya mahubiri katika vyuo vya kidini na katika mienendo ya wanazuoni wakubwa, ameongeza kuwa: Kipaumbele cha mahubiri miongoni mwa majukumu ya vyuo vya kidini kiliongezeka maradufu baada ya kuasisiwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa sababu kuanzishwa mfumo wa kisiasa uliosimama kwenye msingi wa dini nchini kuliongeza uhasama wa maadui wenye kiburi dhidi ya Uislamu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema imani ya wananchi ni nguzo ya uthabiti wa mfumo wa Kiislamu na kuongeza kuwa kulinda mfumo huo na kwa hakika kulinda imani ya watu ni wajibu mkubwa zaidi. Amesema katika zama za sasa mahubiri yanayofanyika kwa kutumia mbinu za kielimui na zana za kisasa, ikiwa ni pamoja na mitandao na akili bandia yameimarika sana, hivyo akili pia inahukumu kwamba  mahubiri sahihi yanapaswa kupewa kipaumbele cha kwanza katika kukabiliana na upanga unaomwaga damu wa propaganda za maadui.

Ayatullah Khamenei ameitaja kambi ya maadui wa mfumo wa Kiislamu inayojiita kuwa demokrasia huria, kuwa ni mrengo wa kueneza uongo na upotofu na huku akiashiria uzoefu na ukweli wa historia ya karibuni amesema: Mrengo uliosimama dhidi ya watu wa Iran ni mrengo ulio dhidi ya uhuru na fikra huru, unapinga kila aina ya demokrasia ambayo haifungamani na wenye kiburi, na mapambano ya taifa la Iran pamoja na mfumo wa Kiislamu dhidi ya mrengo huo ni mapambano ya kistaarabu na ya kimataifa.

Ameashiria hali ya kusikitisha ya watu wa Ukraine na kusema ni uthibitisho wa kuendelea ukoloni na uporaji wa nchi za Magharibi. Amesema: "Watu wa Ukraine wanapaswa kuuawa kwa sababu maslahi ya makampuni ya utengenezaji silaha na mauzo ya nchi za Magharibi yamo katika kuendelezwa vita vya Ukraine."

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, hii leo nchi za Magharibi ni dhaifu na zinakabiliwa na hatari kubwa kuliko wakati mwingine wowote. Amesisitiza kuwa: "Marekani ni mkusanyiko wa mashetani na maovu katika nyuga mbalimbali za kisiasa, uhasama na mataifa mengine, makabiliano na taifa la Marekani lenyewe, ubaguzi wa rangi, utovu wa maadili ya kijinsia, uhalifu na ukatili".

4154540

Habari zinazohusiana
captcha