IQNA

Kiongozi Muadhamu ahimiza uenezaji wa mafundisho ya Qur'ani katika jamii

17:34 - April 26, 2025
Habari ID: 3480598
IQNA – Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa wito wa kueneza mafundisho ya Qur'ani Tukufu katika jamii huku akipongeza juhudi za shughuli za Qur'ani zilizofanyika nchini Iran wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. 

“Mwaka huu, Alhamdulillah, mwezi wa Ramadhani, kwa kweli ulikuwa mwezi wa Qur'ani. Katika nchi nzima, kwa juhudi zenu, ndugu kutoka sekta zote, ndani na nje ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB), mioyo ya watu ilikuwa pamoja na Qur'ani Tukufu,” alisema Ayatullah Seyyed Ali Khamenei siku ya Alhamisi katika kikao cha maombolezo cha kumbukumbu ya kuuawa shahidi kwa Imam Sadiq (AS). 

Alikuwa akiashiria programu mbalimbali za Qur'ani zilizofanyika kote nchini, ikiwemo kipindi maarufu cha televisheni cha 'Mahfel' kilichorushwa kupitia IRIB TV 3.

“Hili ndilo tunalohitaji. Hili ndilo haswa taifa letu linahitaji—ndilo vijana wetu wanahitaji,” aliongeza Kiongozi Muadhamu.

“Nilipoona vijana wameketi wakisoma Qur'ani kwa Tarteel, au Hafidh akisoma kwa moyo, niliingiwa na furaha na nikamshukuru Mwenyezi Mungu, Alhamdulillah Rabb al-'Alamin,” alisema Ayatullah Khamenei. 

“Hata hivyo, linapokuja suala la Qur'ani, bado kuna kazi kubwa ya kufanywa, kazi inayopaswa kufanywa,” aliendelea, akisema, “Tunapaswa kueneza maana za Qur'ani, hii bahari kubwa na yenye kina kirefu, kwa watu wetu na wale wanaoisoma."

Msimu wa kwanza wa kipindi cha 'Mahfel' kilirushwa katika mwezi wa Ramadhani mwaka wa 2023, huku misimu iliyoendelea ikirushwa mnamo 2024 na 2025. Kipindi hicho kimepokelewa vyema na mamilioni ya watazamaji nchini Iran na katika mataifa mengine. 

Maqari mashuhuri wa Kiirani Ahmad Abolqassemi na Hamed Shakernejad wamekuwa miongoni mwa waendeshaji wa kipindi hicho katika misimu yote iliyotangazwa hadi sasa.

3492832

Habari zinazohusiana
captcha