IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Wanachuo wanapaswa kuleta mabadiliko akilini kulingana na uhalisia wa jamii ya Iran

22:07 - April 19, 2023
Habari ID: 3476890
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: kinyume na matakwa ya adui, jamii ya wanachuo inapaswa kuleta mabadiliko akilini kulingana na uhalisia wa jamii ya Iran na kisha kuleta mabadiliko akilini kulingana uhalisia wa dunia na kuelekeza uono na juhudi zake katika upeo wa malengo ya muda mrefu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, jana jioni alikuwa na mkutano mkubwa na zaidi ya wanachama elfu moja wa jumuiya na wanaharakati mbalimbali wanafunzi wa vyuo vikuu.

 

Akihutubia hadhara hiyo, Ayatullah Khamenei alisema, mwanachuo, harakati zake na mambo anayopigania ni fursa na kitu cha thamani kwa nchi, na akasisitiza tena ulazima wa kuimarisha misingi na miundombinu ya kimaarifa ya wanachuo na asasi za wanachuo huku akiutaja uadilifu kuwa msingi wa maarifa na akabainisha kwamba kielelezo muhimu cha uadilifu ni kuondoa ukosekano wa usawa.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ameutaja uhuru wa binafsi kuwa msingi mwingine wa maarifa na akasema: Katika mtazamo wa Uislamu, "kuondokana na mfumo na matashi ya vitu vya kimaada" ndicho kipengee muhimu zaidi cha uhuru wa binafsi, kinachofungua njia ya maendeleo na utukukaji na kujitoa kwenye pingu za udororaji, mgando wa mawazo, kuchanganyikiwa, kurudi nyuma, madola makuu yenye nguvu, madikteta na vizuizi vinginevyo.

 

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake mbele ya hadhara ya wanachuo Ayatullah Khamenei alisema, hakubaliani na watu wanaoziona harakati za wanachuo kuwa ni tishio, na akasisitiza kwamba: rai yangu hasa na isiyo na shaka ni kwamba mwanachuo, harakati zake, mambo anayopigania, kujihisi kwake kuwa ana masuulia kuhusiana na masuala ya nchi, hamu na shauku yake ya kutatua matatizo na kushiriki kwake kwa hamasa katika matukio ya kijamii, minasaba na hafla za kisiasa ni fursa na kitu chenye thamani.

 

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia pia mkakati wa adui wa kuwafanya wananchi wa Iran wawe na mtazamo mbaya juu ya wao wenyewe na uwezo wao, na akafafanua kwa kusema: ulimwengu wa intaneti ni suala la uhalisia, lakini baadhi ya watu wanakubali kumiminiwa tu habari, maelezo na uchambuzi katika ulimwengu wa intaneti ilhali wanapaswa kufanya jitihada za kueneza katika anga hiyo na mitandao ya kijamii habari na uchambuzi sahihi.

Vilevile Ayatullah Khamenei ameashiria uwezekano wa kuletwa mabadiliko hasi kupitia watu waliopotoka, na kwa hivyo akawausia vijana kufuata njia iliyonyooka na kuimarisha msingi wao wa kidini, kielimu, kiakili na kiirada na akasema: kila mtu atakayeijenga zaidi nafsi yake katika masuala haya, ataweza kutoa mchango athirifu zaidi katika siku za usoni.

4135229

Habari zinazohusiana
captcha