IQNA

Siasa

Kiongozi Muadhamu baada ya kupiga kura: Wafurahisheni marafiki na wakatisheni tamaa maadui

11:08 - March 01, 2024
Habari ID: 3478434
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amepiga kura yake katika dakika za awali za upigaji kura kwa ajili ya awamu ya 12 ya Majlisi ya Ushauuri ya Kiislamu (Bunge) na awamu ya 6 ya Baraza la Wataalamu wa Uongozi.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema baada ya kupiga kura yake kwamba, macho ya watu wengi na watu wenye nafasi ya kisiasa duniani wanaitazama Iran.

Akiwahutubia wananchi wa Iran, Kiongozi Muadhamu amsema: Jueni kwamba, leo macho ya watu wengi na watu wenye nafasi ya kisiasa duniani wanaitazama Iran hivyo basi, basi wafurahisheni marafiki zenu na wakatisheni tamaa maadui na wanaolitakia mabaya taifa hili.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran akijibu swali kuhusu wale ambao bado wanasitasita kushiriki katika uchaguzi huo amesema: Hakuna haja ya kufanya istikhara katika jambo la kheri.

Kiongozi Muadhamu, amemuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba siku ya uchaguzi iwe siku yenye baraka kwa taifa la Iran na kwamba uchaguzi huo ufikie matokeo yanayotarajiwa na kuishia kwa manufaa ya taifa la Iran.

Uchaguzi wa duru ya 12 ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) na Baraza la Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu unafanyika leo Ijumaa kote nchini ambapo wagombea wanawania viti 290 vya Bunge na 88 vya Baraza la Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa nchi.

Zaidi ya wagombea 15,200 wanawania viti 290 vya ubunge, 30 kati ya hivyo ni vya mji mkuu, Tehran, ambao unatambuliwa kuwa jimbo kubwa zaidi la uchaguzi nchini.

3487381

captcha