IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Uwezo mkubwa wa utambuzi na azma thabiti ni sifa mbili kuu za kuigwa za Hadhrat Hamza

15:45 - February 04, 2022
Habari ID: 3474886
TEHRAN (IQNA)- Matini ya Hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyotoa katika mkutano na waandaaji wa kongamano la Hadhrat Hamza AS, uliofanyika tarehe 25 ya mwezi uliopita wa Januari ilitolewa katika kongamano hilo lililofanyika jana katika mji wa Qom.

Katika hotuba yake hiyo kwa waandaaji wa kongamano hilo, mbali na kuwashukuru waandaaji hao wa kongamano la kumuenzi Hadhrat Hamza bin Abdul Muttalib, ami wa bwana Mtume SAW, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alisema, maandiko ya kielimu na kiuhakiki ya kongamano hilo kunaandaa mazingira mwafaka ya kujengea utamaduni, ruwaza na mfano wa kuigwa wa shakhsia huyo mkubwa wa Uislamu.

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, licha ya mchango mkubwa aliotoa Hadhrat Hamza katika historia ya Uislamu, hasa katika Hijra ya kuelekea Madina na ushujaa wake katika vita na makafiri, lakini shakhsia huyo mwenye thamani hajulikani; na kwa hivyo inapasa maisha ya shakhsia huyo adhimu pamoja na masahaba wengine wakubwa wa Mtume SAW ambao hawajluikani, kama Ammar, Salman, Miqdad na Jaafar bin Ab Talib yabainishwe katika sura ya tasnia ya sanaa na filamu.

Halikadhalika, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, lengo la Bwana Mtume SAW la kuwaamuru wanawake wa Madina wamlilie Hadhrat Hamza baada ya kuuawa shahidi na kumtaja yeye kuwa ni Bwana wa Mashahidi, lilikuwa ni kuonyesha ruwaza na mfano wa kuigwa kwa ajili ya historia yote na kwa Waislamu wote wa shakhsia huyo shujaa na aliyekuwa na moyo wa kujitolea; na akasisitiza kwamba: sifa mbili muhimu ambazo ni mfano wa kuigwa katika shakhsia ya Hadhrat Hamza ni "uwezo mkubwa wa utambuzi" na "irada imara na azma thabiti".

4033513

captcha