IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Hija ni tukio la kimataifa na miadi ya dunia yenye manufaa ya dunia na Akhera

18:28 - May 17, 2023
Habari ID: 3477008
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza katika kikao cha maafisa wanaoshughulikia ibada ya Hija kwamba: Hija ni tukio la kimataifa na miadi ya dunia yenye manufaa mengi ya dunia na Akhera.

Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kwamba, kuwa na mtazamo sahihi kuhusu Hija na kuelewa umuhimu wa faradhi hiyo ni jambo muhimu sana na kusisitiza kuwa: Hija ni suala la kimataifa na la kiustaarabu ambalo lengo lake ni kustawisha Umma wa Kiislamu, kuzikurubisha zaidi nyoyo za Waislamu na kuunganisha Umma wa Kiislamu dhidi ya ukafiri, dhulma, ubeberu na masanamu ya kibinadamu na yasiyo ya kibinadamu.

Akizungumzia manufaa ya kidunia na ya Akhera ya ibada hiyo adhimu, Ayatullah Khamenei amesema: Kama hakuna Hijja, Umma wa Kiislamu utaporomoka.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja umoja wa Umma wa Kiislamu na kukabiliana na mashetani wenye kiburi na mabeberu kuwa ni miongoni mwa malengo hayo na kuongeza kuwa: Miongoni mwa manufaa mengi ya duniani ya Hija ni kwamba katika mkusanyiko huo mkubwa, Waislamu wanatangaza uwepo na nguvu zao mbele ya utawala wa Kizayuni na ushawishi wa madola ya kibeberu, na wanasimama kidete dhidi ya madhalimu wa dunia.

Ayatullah Ali Khamenei ameashiria ulazima wa kujua masuala ya dunia na hali ya mataifa ya Kiislamu na kusema: Siku za Hija ni fursa adhimu ya kufahamiana na mataifa na kuelewa vyema masuala ya kimataifa ili habari za uongo za vyombo vya habari na mashirika ya habari zisiwapoteshe watu na kuwaweka mbali na ukweli na hali halisi ya ulimwengu.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema ujahili na kutokuwa na habari kuhusu yanayojiri duniani ni sababu ya kuangamia kwa jamii yoyote ile na kuongeza kuwa: Watu na viongozi wanapaswa kuyapa umuhimu mkubwa masuala ya kutambua malengo, mbinu, sera, nguvu na udhaifu wa adui.

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa: Iwapo tutafahamu vyema masuala ya kimataifa, tutaweza kuelewa lengo halisi la adui na sababu ya kung'ang'ania kwake baadhi ya masuala, kama ilivyokuwa katika masuala mengi, ambako maafisa wamekuwa waangalifu na wametenda ipasavyo, na matokeo yake ni maendeleo mazuri sana ya Iran katika masuala ya kieneo na kimataifa, ambayo yameikasirisha Marekani.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Nchi zinazodai kustaarabika, kwa hakika hazijanusa hata harufu ya ustaarabu, na zingali zinashughulishwa na kadhia ya watu weusi na weupe, na wazungu na wasio wazungu; na zinathamini zaidi wanyama wao wa ndani kuliko binaadamu wengine; na hapana shaka kuwa kuzama mara kwa mara wahamiaji baharini ni uthibitisho wa ukweli huu.

4141388

Habari zinazohusiana
captcha