IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Kutomuogopa adui na kukabiliana naye ni katika maamrisho muhimu ya Qurani Tukufu.

10:39 - April 26, 2020
Habari ID: 3472706
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kutomuogopa adui na kusimama kidete dhidi yake ni katika maamrisho na maelekezo muhimu ya Qurani Tukufu.

Ayatullah Sayyed Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuhusu nukta hiyo muhimu ya Qur'ani jana Jumamosi mjini Tehran katika siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakati wa mahafali ya kujikurubisha na Qur'ani Tuklufu. Mahalafali hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mossala wa Tehran na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alihudhuria kwa njia ya mawasiliano ya moja kwa moja ya video katika Husseiniya ya Imam Khomieni MA.

Kiongozi Muadhamu aliongeza kuwa, njia pekee ya kuinusuru jamii ya wanadamu kuondokana na dhulma, ubaguzi, maonevu, vita, ukosefu wa usalama, na kutoheshimiwa thamani za kiutu ambako kumeshuhudiwa katika kipindi chote cha historia, ni kufuata kivitendo mafundisho ya Qurani Tukufu.

Ayatullah Khamenei amefafanua kuhusu nukta hiyo kwa kusema: "Sehemu moja ya maamurisho ya Qur'ani Tukufu ni kuhusu namna ya kuishi; na iwapo maisha yatakuwa kwa msingi wa uchu wa madaraka, pesa na shahawa, basi mwanadamu atakaosa kuishi maisha halisi katika dunia na akhera. Hatahivyo iwapo mwanadamu atapanga maisha yake katika dunia kwa msingi wa kutenda mema sambamba na kufaidika na yaliyoko duniani, basi bila shaka atafika katika malengo halisi na ya ukweli ya maisha."

Amebainisha kuwa, Qurani Tukufu imemfundisha mwanadamu kutumia utajiri na uwezo wake wote kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wanadamu wenzake, na kuwasaidia watu wenye mahitaji katika jamii.

Ayatullah Khamenei alibainisha kuwa "njia pekee ya kuinusuru jamii ya wanadamu kuondokana na dhulma, ubaguzi, maonevu, vita, ukosefu wa usalama, na kutoheshimiwa thamani za kiutu ambako kumeshuhudiwa katika kipindi chote cha historia, ni kufuata kivitendo mafundisho ya Qurani Tukufu."

Ayatullah Khamenei katika hotuba yake ameongeza kuwa kuwa, 'kujizuia kuwaamini na kujikurubisha kwa madhalimu' kuzingatia usawa, uadilifu na insafu katika maisha' na 'kutofanya khiana kuhusu amana' ni kati ya maamurhisho mengine muhimu ya Kiislamu. Aliongeza kuwa: "Kuiogopa Marekani kutakuwa na matokeo machungu. Katika miaka ya nyuma tuliona namna ambayo baadhi ya serikali zilikumbwa na matatizo makubwa kutokana na kuiogopa Marekani."

Kadhalika Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu sambamba na kutoa mkono wa kheri na fanaka kwa Waislamu wote kote duniani kwa mnasaba wa kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani, ametoa wito kwa umma wa Kiislamu kustafidi na mwezi huu kwa kujikurubisha zaidi kwa Mola, kwa lengo la kuinususu jamii ya mwanadamu.

3894129

Habari zinazohusiana
captcha