IQNA - Bendera ya kijani kibichi ya Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS), Imam wa Nane wa Waislamu wa madhehebu ya Shia huko Mashhad ilibadilishwa na nyeusi kuashiria kuanza kwa siku tano za maombolezo ya kitaifa mnamo Mei 20, 2024, kufuatia vifo vya kusikitisha vya rais wa Iran, waziri wa mambo ya nje na ujumbe wa walioandamana nao katika ajali ya helikopta. Shahidi Raisi ni mwenyeji wa mji wa Mashhad na aliwahi wakati moja kuwa msimamizi wa Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS).
Photos and video by new.razavi.ir