IQNA

Maombolezo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran azikwa katika Haram ya Shahd Abdul Adhim (AS), mkoani Tehran

19:07 - May 23, 2024
Habari ID: 3478877
IQNA-Mwili wa Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliyekufa shahidi katika ajali ya helikopta iliyotokea Jumapili iliyopita kaskazini magharibi mwa nchi umezikwa leo katika Haram ya Shah Abdul Adhim Hassani (AS) katika mji wa Shahre-Rey, eneo la kusini la makoa wa Tehran.

Maelfu ya wananchi wa Waislamu wa Iran wamejitokeza kuuaga na kuuzika mwili wa mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Jamhuri ya Kiislamu. Kadhalika maafisa wa ngazi za juu wa Iran wamehudhuria maziko hayo mjini Rey.

Miongoni mwa shakhsia walioshiriki kwenye maziko ya Amir-Abdollahian ni aliyekuwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran, Mohammad Javad Zarif, Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB), Peyman Jebeli, Mohammad Eslami, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI), Dakta Ali Larijani, aliyekuwa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), na Sayyid Abbas Araqchi, Katibu wa Baraza la Kistratajia la Mahusiano ya Kigeni la Iran.

Viongozi wengine wa ngazi za juu walioshiriki katika shughuli ya kuuaga mwili wa Amir-Abdollahian ni Ali Bagheri Kani, Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf na Nasser Kan'ani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, miongoni mwa mwengine.

Shahidi Amir-Abdollahian daima amekuwa akitilia mkazo kusitishwa mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina.

Aidha atakumbukwa kwa kufanya kazi kubwa ya kufufua na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kibiashara, kiuchumi na kiutamaduni wa Iran na nchi mbalimbali duniani hasa za Afrika na mataifa ya Kiislamu na Kiarabu ya Asia Magharibi na Ghuba ya Uajemi.

Helikopta iliyokuwa imembeba Sayyid Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Jumapili jioni Mei 19, 2024 ilipata ajali ilipokuwa ikirejea kutoka kwenye hafla ya ufunguzi wa bwawa la Qiz Qalasi kwenye mpaka wa pamoja wa Iran na Jamhuri ya Azerbaijan.

Wakati helikopta hiyo ilipokuwa inaelekea mji wa Tabriz, ilianguka katika eneo la Varzghan mkoani Azarbaijan Mashariki, kaskazini-magharibi mwa Iran. Ndani yake walikuwemo pia Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje, Imam wa Ijumaa wa Tabriz, Gavana wa Azarbaijan Mashariki na watu wengine; na wote pamoja wakaifika hadhi tukufu ya kufa shahidi.

 

4217891

 

Habari zinazohusiana
captcha