IQNA

Ulimwengu wa Kiislamu

'Hasara kwa Umma wa Kiislamu': Mwanazuoni asema kuhusu kufa shahidi Rais wa Iran na wenzake

22:24 - May 26, 2024
Habari ID: 3478888
IQNA - Mwanazuoni wa Lebanon anasema kufa shahidi Rais wa Iran hayati Ebrahim Raisi na Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian ilikuwa hasara kwa Umma wa Kiislamu.

"Ayatullah Raisi alikuwa na sifa ya kipekee na alifuata kwa uaminifu kanuni za Uislamu na mafundisho ya babu yake, Mtume Muhammad (SAW)," Sheikh Zuhair Jaid, mratibu wa Harakati ya Kiislamu ya Lebanon ya Amal, aliliambia Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) siku ya Jumapili.

"Raisi alikuwa mtumishi aliyejitolea na mpenzi wa taifa lake, mfuasi mkubwa wa watu wanaokandamizwa na walio huru duniani, hususan taifa la Palestina," aliongeza.

Raisi pia alitetea harakati zote muqawama (mapambano ya Kiislamu) katika mapambano yao dhidi ya dhulma na uchokozi wa utawala ghasibu wa Israel na Marekani, aliongeza mwanazuoni huyo.

Pia alimsifu Amir-Abdollahian, akibainisha kwamba mwanadiplomasia huyo marehemu mara kwa mara alikuwa akiunga mkono vikosi vya muqawama.

"Alipata cheo cha waziri wa mambo ya nje wa mhimili wa muqawama," Sheikh Jaid alisema.

Zaidi ya nafasi yake kama Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran, alijitokeza katika jukwaa la kimataifa kama mshika bendera wa muqawama, alisema mwanazuoni huyo.

"Amir-Abdollahian hakuchoka kutetea wanamapambano wa Kiislamu Palestina na Gaza," alisema.

"Kupoteza Raisi na Amir-Abdollahian, na walioandamana na si msiba mzito tu kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran bali pia hasara kubwa kwa Umma wote wa Kiislamu," aliongeza.

  "Watu wa Lebanon, Palestina, Gaza, na wapiganaji wa vikosi vya muqawama wa­­lihisi hasara hii, haswa wakati ambapo taifa la Palestina lilikabiliwa na vita vya mauaji ya adui wa Kizayuni na viongozi waovu wa Amerika," Sheikh Jaid alibainisha.

Helikopta iliyokuwa imembeba Raisi Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Amir-Abdollahian, kiongozi wa Swala ya Ijumaa ya Tabriz Ayatollah Mohammad Ali Al-e-Hashem, Gavana wa Azarbaijan Mashariki Malek Rahmati, kamanda wa kikosi cha usalama cha rais, marubani wawili na walinzi ilianguka mkoa wa kaskazini-magharibi wa Azarbaijan Mashariki mnamo Mei 19, 2024. Miili yao ilipatikana siku ya Jumatatu baada ya msako wa usiku mzima katika eneo lililokuwa na hali mbaya ya hewa.

Iran iliadhimisha siku tano za maombolezo ya kitaifa. Shahidi Raisi Raisi alizikwa katika Haram Takatifu ya Imam Ridha  (AS) huko Mashhad naye Shahidi Amir-Abdollahian akazikwa kwenye Haram Takatifu ya Hadhra Abdul  Adhim  Hassani (AS) huko Rey, kusini mwa Tehran.

3488498

Habari zinazohusiana
captcha