Hafla hiyo ilifanyika katika katika Ukumbi wa Husseiniya ya Imam Khomeini mjini Tehran tarehe 25 Mei 2024, ambapo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alijumuika na wananchi wa matabaka mbali mbali, maafisa wa serikali na mabalozi wa nchi za kigeni.
Helikopta iliyokuwa imembeba Raisi Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Amir-Abdollahian, kiongozi wa Swala ya Ijumaa ya Tabriz Ayatollah Mohammad Ali Al-e-Hashem, Gavana wa Azarbaijan Mashariki Malek Rahmati, kamanda wa kikosi cha usalama cha rais, marubani wawili na walinzi ilianguka mkoa wa kaskazini-magharibi wa Azarbaijan Mashariki mnamo Mei 19, 2024. Miili yao ilipatikana siku ya Jumatatu baada ya msako wa usiku mzima katika eneo lililokuwa na hali mbaya ya hewa.
Iran iliadhimisha siku tano za maombolezo ya kitaifa. Shahidi Raisi Raisi alizikwa katika Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad naye Shahidi Amir-Abdollahian akazikwa kwenye Haram Takatifu ya Hadhra Abdul Adhim Hassani (AS) huko Rey, kusini mwa Tehran.