IQNA

Madina: Jukwaa la mtandaoni lazinduliwa kwa watoa huduma ya Iftar katika msikiti wa Mtume Muhammad (SAW)

14:53 - February 05, 2025
Habari ID: 3480168
IQNA – Mamlaka kuu ya kusimamia masuala ya msikiti mkuu wa Makka na Msikiti wa Mtume Muhammad (SAW)  imezindua jukwaa la mtandaoni kwa watoa huduma ya Iftar katika Msikiti wa Mtume Muhammad (SAW)  jijini Madina, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha wanahakiki na kusasisha taarifa zao kabla ya kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.  

 

Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, watoa huduma wanatakiwa kukamilisha mchakato wa kusasisha taarifa zao, kusaini mikataba na makampuni ya upishi yaliyoidhinishwa, na kuzingatia miongozo iliyowekwa kwa huduma ya iftar.

Shirika la Habari la Saudi (SPA) limeripoti kuwa baada ya kukamilika kwa mchakato huu wa kusasisha taarifa, orodha ya makampuni yaliyoidhinishwa itatangazwa, kuruhusu watoa huduma kumalizia mikataba yao na kupatiwa ruhusa za kielektroniki kwa ajili ya utoaji wa huduma.

 Mfumo Kama Huu Ulizinduliwa Makka Mwezi Uliopita

Katika hatua nyingine kama hii mwezi uliopita, mamlaka hiyo ilizindua jukwaa maalum kwa mashirika ya hisani na watu binafsi kutuma maombi ya kutoa huduma ya chakula cha iftar ndani ya Msikiti Mkuu wa Makka wakati wa Ramadhani.

 Mfumo huo unaruhusu waombaji kuchagua maeneo ya kusambaza chakula, ambapo:

Watu binafsi wanaruhusiwa eneo moja pekee

Mashirika ya hisani yanaweza kupewa hadi maeneo 10

Aidha, mamlaka hiyo imehimiza utoaji wa vyakula vyenye kalori chache, vinavyofaa kwa watu wenye magonjwa sugu kama kisukari ili kuhakikisha afya njema ya waumini wanaofuturu ndani ya misikiti hiyo mitakatifu.

 

 

 3491747

 

 

 

 

 

captcha