IQNA

Chuo cha Kiislamu Sarajevo Chaandaa Semina Kuhusu Dhana ya ‘Muda’ Katika Qur’ani

17:08 - November 02, 2025
Habari ID: 3481453
IQNA – Chuo Kikuu cha Gujrat, Kampasi ya Hafiz Hayat, nchini Pakistan kimeandaa semina maalum yenye kichwa cha habari “Dhana ya Muda kwa Mujibu wa Qur’ani Tukufu,” ikiwaleta pamoja wanafunzi kwa ajili ya maarifa ya kiakili na kiroho.

Semina hiyo iliandaliwa na Jumuiya ya Sayansi ya Hayatian (HSSC) kwa ushirikiano na Idara ya Masuala ya Wanafunzi wa chuo hicho, kwa lengo la kukuza uelewa wa kina kuhusu nafasi ya muda katika mafundisho ya Kiislamu.

Mgeni rasmi alikuwa msomi mashuhuri wa Kiislamu, Sheikh Tahir Jaleel Azeemi, huku kikao kikiongozwa na Mratibu wa HSSC, Dkt. Zahid Anwar.

Katika hotuba yake, Sheikh Azeemi alisisitiza kuwa Uislamu unahimiza matumizi ya akili na hekima badala ya kufuata kwa upofu. “Uislamu ni dini ya tafakuri na busara, si ya kurithi bila kuelewa,” alieleza.

Alifafanua dhana mbalimbali za muda zilizotajwa katika Qur’ani Tukufu kama vile saat, waqt, dahr, na al-asr, akieleza uhusiano wake na imani pamoja na hali ya kumtambua Mwenyezi Mungu.

Semina ilihitimishwa kwa usomaji wa Qur’ani Tukufu na maonyesho ya naat, kisha zawadi za kumbukumbu zilitolewa na Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma kwa Wanafunzi, Khurram Irshad.

3495221

Habari zinazohusiana
Kishikizo: pakistan qurani tukufu
captcha