Ayatullah Khamenei ametoa kauli hiyo Jumatatu kupitia ujumbe kwa wananchi wa Iran, kufuatia maandamano ya nchi nzima ambako washiriki walilaani machafuko yanayoungwa mkono na mataifa ya kigeni na wakathibitisha upya uungaji mkono wao kwa Jamhuri ya Kiislamu.
Ameongeza kuwa: “Enyi wananchi waheshimiwa wa Iran, leo mmetimiza jukumu kubwa na mkaweka alama ya siku ya kihistoria. Mikusanyiko hii mikubwa, iliyojaa azma thabiti, imevuruga njama za maadui wa kigeni zilizotarajiwa kutekelezwa kupitia vibaraka wa ndani.”
Kiongozi Muadhamu amebaini kuwa maandamano hayo yaliwaonyesha maadui “azma na utambulisho” wa taifa, na yakawa pia onyo kwa maafisa wa Marekani “kuacha udanganyifu wao na kusitisha kutegemea vibaraka wasaliti.”
Ayatullah Khamenei amewataja wananchi wa Iran kuwa “wenye nguvu, madhubuti na wenye ufahamu,” akisema kuwa daima wanajitokeza na kubaki macho nyakati za misukosuko.

Maandamano ya amani kulalamikia ugumu wa kiuchumi wiki iliyopita yaligeuka kuwa vurugu, yakichochewa na matamshi ya viongozi wa Marekani na Israel, huku makundi yenye silaha yakiharibu mali ya umma na kusababisha mauaji na majeruhi miongoni mwa raia na maafisa wa usalama.
Vyombo vya usalama na mahakama vinasema vimefanikiwa kuvunja baadhi ya mitandao ya watu wenye silaha na kuwakamata watuhumiwa wenye uhusiano wa kigeni wakati wa machafuko hayo.
Wakati huohuo, Rais Masoud Pezeshkian amepongeza uwepo “wa kishujaa na wa kuvutia” wa mamilioni ya Wairani katika maandamano ya kitaifa dhidi ya ghasia za hivi karibuni, akisema mwitikio huo mkubwa umezima “mipango miovu” ya maadui wa kigeni na vibaraka wao.
Amesema maandamano hayo ni ishara ya “umakinifu na uwajibikaji usio na kifani” katika kutetea misingi ya dini na utaifa mbele ya “maadui wakandamizaji na magaidi wanaotegemea nguvu za nje.”
Pezeshkian amesisitiza kuwa umoja ulioonekana katika mikoa yote umeunda ngao dhidi ya “njia za uhalifu” za Marekani, washirika wake na utawala wa Israel.
Akaongeza kuwa maandamano hayo yameifanya serikali kuwa “na dhamira iliyoimarika zaidi” kukabili changamoto za nchi kutoka ndani.
Katika ujumbe wake kwa taifa kufuatia maandamano ya Jumatatu, rais alitoa shukrani za dhati kwa “ustahimilivu na msimamo” wa wananchi mbele ya misukosuko na kuingiliwa na nguvu za kigeni.
Maandamano yalianza mapema saa 3 asubuhi kote nchini, huku ikiripotiwa kuwa takribani watu milioni tatu walijitokeza Tehran pekee.

4328325