IQNA

Mamilioni ya Wairani Waungana Kulaani Ugaidi wa Kizayuni na Kimarekani

10:04 - January 13, 2026
Habari ID: 3481796
IQNA – Mamilioni ya wananchi nchini Iran waliandamana Jumatatu kulaani ghasia za hivi karibuni zilizochochewa na makundi ya kigaidi yanayodaiwa kuungwa mkono na Marekani na utawala wa Kizayuni.

Maandamano hayo yalifanyika katika miji na miji mbalimbali, ikiwemo Tehran, chini ya kaulimbiu ya “Umoja wa Kitaifa na Kuheshimu Amani na Urafiki.”

Washiriki walilaani vikali utawala wa Kizayuni, Marekani na washirika wao wanaotuhumiwa kutekeleza vitendo vya ugaidi na uharibifu ndani ya Iran katika siku za karibuni.

Aidha, walionyesha kuchukizwa kwao na watu waliovunjia heshima Kitabu Kitukufu cha Qur’ani na kuvamia misikiti wakati wa ghasia hizo.

Waandamanaji, wanaokadiriwa kufika milioni tatu jijini Tehran pekee, walisisitiza pia kuunga mkono vikosi vya ulinzi na usalama vya nchi.

Wakiwa wamebeba mabango yenye maandishi kama “Ya Hussein” na “Labbayka Ya Khamenei,” walipaza kauli mbalimbali za kisiasa dhidi ya Israel, Marekani na makundi wanayoyaita wanafiki.

Viongozi waandamizi wa serikali, akiwemo Rais Masoud Pezeshkian, Spika wa Bunge Mohammad Bagher Ghalibaf, Mkuu wa Mahakama Hujat-ul-Islam Gholam Hossein Mohseni Ejei, pamoja na Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa Ali Larijani, walijumuika na wananchi katika maandamano hayo.

Soma zaidi.

               Kiongozi Muadhamu:: Kujitokeza wananchi katika maandamano ya kitaifa Iran kumevuruga njama za maadui

Katika tukio lililotangulia, ghasia zilizotokea Alhamisi na Ijumaa ziliripotiwa kusababisha vifo vya raia na maafisa wa usalama, huku mali za umma na binafsi zikiharibiwa katika baadhi ya miji.

Wahalifu hao walivunja miundombinu, kuziba barabara, kushambulia majengo ya serikali na vituo vya polisi, na kujeruhi au kuua maafisa wa usalama.

Pia walichoma moto misikiti kadhaa na kukivunjia heshima Kitabu Kitukufu cha Qur’ani.

4328246

captcha