IQNA

Adui anatambua dhamira ya Qur’ani ya kujenga ustaarabu

15:36 - January 14, 2026
Habari ID: 3481799
IQNA – Mwanazuoni wa Kiirani amesema kuwa Qur’ani Tukufu imetangaza wazi kuwa jukumu lake ni kuanzisha ustaarabu mpya, na adui analijua hilo.

Mohammad Sadeq Elmi, profesa katika Chuo Kikuu cha Ferdowsi mjini Mashhad, aliyasema haya katika mahojiano na IQNA kuhusu machafuko ya hivi karibuni nchini Iran ambamo magaidi wanaopata himaya ya shirika la kijasusi la Israel, Mossad, na Marekani walivunjia heshima nakala za Qur’ani Tukufu na misikiti pamoja na maeneo matukufu.

Amesema kuwa kukabiliana na Kitabu Kitakatifu kwa namna hii na kukivunjia heshima kunaonyesha kuwa maadui wana hofu nacho.

Akaongeza kuwa kufichua ujinga wa maadui ndicho chanzo cha uadui wao dhidi ya Qur'ani Tukufu.

Elmi alisema uhasama huu umekuwepo katika zama mbalimbali, na wamejaribu kila njia kudhoofisha na kuharibu hadhi ya Kitabu Kitakatifu cha Uislamu, lakini juhudi zao zote zimegonga mwamba.

Alisema kuwa wakati Mtume Mtukufu Muhammad (SAW) alipokuwa akisoma Qur’ani huko Makka, washirikina walikuwa wakipiga kelele ili watu wasimsikie. Tukio kama hilo limejirudia mara nyingi katika nyakati tofauti na kwa mbinu mbalimbali.

Alipoulizwa kuhusu wajibu wa jamii ya wana-Qur’ani katika kukabiliana na mashambulizi ya adui dhidi ya Kitabu Kitakatifu, Elmi alisema wanapaswa kuongeza uelewa na elimu yao kuhusu mafundisho ya Qur’ani na kujitahidi kuyatekeleza malengo ambayo Kitabu Kitakatifu kimeyaweka.

Waandamanaji wenye vurugu waliharibu mali za umma na binafsi katika miji kadhaa nchini Iran siku ya Alhamisi na Ijumaa, na kuua baadhi ya raia pamoja na maafisa wa usalama, huku wengine wakijeruhiwa.

Walivunja mali za umma, wakaziba barabara, wakashambulia majengo ya serikali na vituo vya polisi, na kuua au kujeruhi idadi ya maafisa wa usalama na sheria.

Pia walichoma moto misikiti kadhaa na kuvunjia heshima nakala za Qur’ani Tukufu.

4328341

Kishikizo: iran maandamano
captcha