
Katika mji mkuu wa Iran, Tehran waombolezaji wakiwa wamebeba picha za mashahidi, bendera ya Iran na picha za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu walisikika wakipiga nara za "Mauti kwa Marekani" na "Mauti kwa Israel". Mjini Tehran, shughuli ya kuwaaga mashahidi wa ulinzi na raia wengine waliouawa shahidi na makundi ya kigaidi yanayounga mkono na Marekani na Israel katika machafuko ya hivi karibuni hapa nchini ilianzia katika Chuo Kikuu cha Tehran ambapo mbali na raia wa kawaida maafisa wa serikali na kijeshi pia wamehudhuria shughuli hiyo.
Wakati huo huo, shughuli kama hiyo ya mazishi ya mashahidi wa raia wa kawaida na walinzi wa usalama walioauawa shahidi katika uhalifu wa mamluki wa Kizayuni na Marekani zimefanyika katika miji mengine ya Iran, ikiwa ni pamoja na Isfahan, Bushehr, na Mashhad na kwingineko na kushuhudiwa ushiriki mkubwa.
Maandamano ya amani kulalamikia ugumu wa kiuchumi wiki iliyopita yaligeuka kuwa vurugu, yakichochewa na matamshi ya viongozi wa Marekani na Israel, huku makundi yenye silaha yakiharibu mali ya umma na kusababisha mauaji na majeruhi miongoni mwa raia na maafisa wa usalama.
Vyombo vya usalama na mahakama vinasema vimefanikiwa kuvunja baadhi ya mitandao ya watu wenye silaha na kuwakamata watuhumiwa wenye uhusiano wa kigeni wakati wa machafuko hayo.
Rais wa Marekani, Donald Trump, ameendelea kutoa kauli zake za kichochezi za kuwaunga mkono wanaobua fuja na ghasia nchini Iran na akatahadharisha kuwa Washington inaweza kuihujumu Iran endapo wale anaodai kuwa eti ni “waandamanaji wa amani” watadhuriwa.
Hapa chini ni picha za mjumuiko huo wa mazishi
4328504