
Aidha unaheshimiwa pia kama msikiti wa kwanza mjini humo ambamo Sala ya Ijumaa iliwahi kuswaliwa ikiwa ni ishara ya nafasi yake ya kihistoria na kiroho.
Msikiti huu ulianzishwa na Sheikh Jafar Abu Mukaram, mwanazuoni mashuhuri wa eneo hilo aliyeacha athari kubwa katika elimu na uongozi wa dini.
Takribani nusu karne iliyopita, msikiti ulifanyiwa ukarabati kupitia mpango wa kuhifadhi maeneo ya kale ya ibada, mradi uliogharimiwa na watu wa Sihat kwa kiasi cha riyali 22,000. Baadaye, Sheikh Abdul Majid Abu Mukaram, mjukuu wa Sheikh Jafar, alianzisha juhudi nyingine za ukarabati zilizolenga kuuingiza msikiti katika muundo wa kisasa bila kupoteza utukufu wake wa kale.
Mnamo mwaka 2022, wakazi wa Sihat walikubaliana kuanza upya ukarabati wa msikiti. Kwa muda wa matengenezo, ibada zote, ikiwemo Sala ya Ijumaa, zilihamishiwa katika Msikiti wa Imam Hassan al-Askari (AS) uliopo eneo la al-Zuhour.
Kabla ya ukarabati wa karibuni, msikiti uliweza kuchukua waumini 1,800, idadi ambayo iliongezeka baada ya marekebisho. Pia una sehemu maalumu ya kuswalia wanawake yenye uwezo wa kuhudumia waumini 100 hadi 150.
Msikiti huu unajulikana kwa harakati zake za kielimu, ikiwemo masomo ya dini na madarasa ya Qur’ani, jambo linaloufanya kuwa kitovu cha malezi ya kiroho katika jamii.
Mji wa Sihat ni miongoni mwa miji muhimu katika Mkoa wa Mashariki, na aghalabu ya wakazi wake ni Waislamu madhehebu ya Shia. Familia nyingi ni za koo za Kiarabu za asili kama vile Khuwaled, Ajman, Hawajer, na Sabila. Mbali na misikiti mikubwa, mji huu pia una idadi kubwa ya Husseiniyya ambazo kimsingi ni vituo vya kidini vya Waislamu wa madhehebu ya Shia vinavyotumika kwa maombolezo, elimu, na mikusanyiko ya kijamii.
4328683