IQNA

Saudia yalitunuku Shirika la Hija la Iran Tuzo ya Labaytum ya Huduma Bora za Hija

15:04 - June 09, 2025
Habari ID: 3480810
IQNA – Shirika la Hija la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetunukiwa Tuzo ya Labaytum kwa ubora katika Huduma kwa Mahujaji.

Shirika hilo limetambuliwa kwa kutoa huduma bora za kiutendaji kwa Mahujaji, hatua iliyolipatia sifa ya kipekee kutoka kwa mamlaka mbalimbali za Kiislamu.

Sherehe ya kufunga msimu wa Hija wa mwaka 2025 ilifanyika jioni ya Jumapili katika jiji takatifu la Makka, ambapo mawaziri na wakuu wa taasisi za Hija kutoka nchi za Kiislamu walihudhuria kwa wingi.

Tukio hilo liliandaliwa na Waziri wa Hija na Umra wa Saudi Arabia, Tawfiq bin Fawzan Al-Rabiah, katika jengo kuu la wizara hiyo nchini humo.

Mkuu wa Shirika la Hijja la Iran Alireza Bayat alipokea Tuzo ya Heshima kutoka Saudi Arabia kwa Huduma Bora kwa Mahujaji.

Tuzo ya kila mwaka ya Labaytum, inayotolewa na Saudi Arabia kwa nchi zinazotoa huduma bora kwa mahujaji wa Hija, ina viwango vinne vya heshima: Almasi, Dhahabu, Fedha, na Shaba.

Tuzo hii hutambua ubora katika upangaji, huduma za afya, mwongozo wa kidini, ustawi wa Mahujaji, matumizi ya teknolojia, na uendeshaji kwa ujumla. Katika hafla ya kifahari iliyofanyika jijini Makka, Iran ilitajwa miongoni mwa washindi wa tuzo ya Shaba, sambamba na Somalia na Tunisia.

Maafisa wa Saudi Arabia walitumia fursa hiyo kuwasilisha mikakati ya maandalizi kwa Hija ya mwaka 2025, wakitoa tathmini ya kitaalamu kuhusu ubora na ufanisi wa huduma zilizotolewa na nchi shiriki. Kwa upande wa mataifa yaliyoibuka na tuzo ya kiwango cha juu zaidi—Almasi—ni Malaysia, Uturuki na Iraq. Dhahabu ikaenda kwa China, Algeria na Singapore, huku Fedha ikichukuliwa na Afrika Kusini, Jordan na Brunei.

Wakati wa hafla hiyo, maafisa wa Saudi walitoa ripoti juu ya maandalizi ya Hija ya mwaka huu, wakieleza tathmini yao ya kitaalamu kuhusu namna nchi mbalimbali za Kiislamu zilivyotekeleza wajibu wao katika kuwahudumia “Wageni wa Mwingi wa Rehema”.

Kwa mara ya kwanza kabisa, Shirika la Hija la Iran lilitangazwa kuwa mshindi wa juu kwa utoaji wa huduma bora kabisa kwa mahujaji.

Tuzo ya Labaytum pamoja na cheti maalum vilikabidhiwa kwa Ali Reza Bayat, mkuu wa Shirika la Hija na Mahujaji la Iran, na Waziri wa Hija wa Saudi Arabia.

4287375

Kishikizo: iran hija saudi arabia
captcha