iqna

IQNA

Mkutano wa 28 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu umeanza leo mjini Tehran kwa kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu na maulamaa wa ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 2684304    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/07

Tehran-IQNA- Waislamu nchini Uganda Jumamosi iliyopita waliadhimisha Maulid (kumbukumbu ya kuzaliwa ) Bwana Mtume Muhammad SAW huku wakitoa wito wa amani na umoja katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki inayokumbwa na migawanyiko miongoni mwa Waislamu.
Habari ID: 2677812    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/06

Tumo katika kumbukumbu ya kufariki dunia Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu Muhammad al-Mustafa SAW. Hii leo imepita zaidi ya miaka 1400 tangu mbora huyo wa viumbe aage dunia; lakini jina la mtukufu huyo pamoja na utajo na shakhsia yake kubwa na adhimu na isiyo na mithili ingali inaleta hamasa katika nyoyo.
Habari ID: 2623557    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/20

Utafiti umeonesha kuwa, jina la Muhammad linaongoza kuitwa watoto nchini Uingereza, ambapo jina hilo limeonekana kupewa watoto wengi zaidi wa kiume kati ya waliozaliwa mwaka huu wa 2014 nchini humo.
Habari ID: 2614518    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/02

Kongamano la Kimataifa la ‘Hatari ya Misimamo Mikali Na Utakfiri Kwa Mtazamo wa Maulamaa wa Kiislamu’ lilianza jana hapa nchini Iran katika mji Mtakatifu wa Qum kusini mwa Tehran kwa kuhuduriwa na mamia ya maulamaa na wanafikra wa Kiislamu kutoka madhehebu ya Shia na Sunni.
Habari ID: 2611223    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/24

Utawala wa Saudi Arabia unapanga kubomoa kaburi la Mtume Muhammad SAW na kuhamisha mwili wake mtukufu katika kaburi lisilojulikana katika hatua ambayo bila shaka itaibua hasira za Waislamu kote duniani.
Habari ID: 1446086    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/09/02

Takwimu mpya katika mji mkuu wa Norway, Oslo zinaoneysha kuwa, Mohammad, jina la Mtume Mtukufu wa Uislamu (SAW) ndio jina mashuhuri zaidi mjini humo.
Habari ID: 1444599    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/08/30

Tarehe 27 Rajab Mwaka wa Tembo na akiwa na umri wa miaka 40, Mtume Muhammad (SAW) alikuwa juu ya kilele cha Mlima Hira, akijishughulisha na ibada ndani ya pango la mlima huo, ambapo ghafla malaika Jibril AS alimteremkia huku akiwa amebeba wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu SW.
Habari ID: 1411465    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/05/27