Akizungumza Alhamisi iliyopita na Televisheni ya NRK, Jørgen Ouren Mkuu wa Shirika la Takwimu nchini Norway (Statistisk Sentralbyrå - SSB) amesema amevutiwa sana na takwimu hizo.
SSB imefanya uchunguzi huo miongoni mwa wanaume waishio mjini Oslo ambapo imebainika kuwa wavulana na wanaume 4,801 wanaitwa Mohammad au majina ambayo chimbuko lake ni Mohammad. Kwa msingi huo, jina Mohammad lilipita jina Jan lenye watu 4,667 na Per 4,155. Hii ni mara ya kwanza kwa jina Mohammad kuongoza kwa umashuhuri katika historia ya mji huo wa Ulaya.
Hivi karibuni pia nchini Uingereza, jina la Mohammad limetangazwa kuwa jina mashuhuri zaidi miongoni mwa wavulana wanaozaliwa Uingereza.
Idara ya Takwimu za Kitaifa Uingereza (ONS) imebaini kuwa zaidi ya watoto 8,000 waliozaliwa nchini humo mwaka 2013 walipewa aina mbali mbali ya jina Mohammad.
Takwimu hizo zinaonyesha kuwa wavulana 3,499 walipewa jina liloandikwa Muhammad; 2,887 Mohammed; 1,059 Mohammad na 561 Muhammed. Kuna aina nyingine 18 za jina Mohammad katika orodha hiyo.
1444187